TANGAZO


Friday, May 30, 2014

HOTUBA YA VIONGOZI WA SERIKALI YA WANAFUNZI WA TAASISI YA AFYA NA TIBA SHIRIKISHI MUHIMBILI (IAHS) KWA YVOMBO VYA HABARI TARE.30/05/2014.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUIAHSSO), Stephano Haule, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuomba kurejeshwa kwa ada ya zamani kwa wanafunzi wa Cheti na Diploma wa chuo hicho, kinachoendeshwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Kulia ni Waziri Mkuu wa MUIAHSSO, Bosco Sombela. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
 Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUIAHSSO), Stephano Haule, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo, na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua habari zilizokuwa zikitolewa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUIAHSSO), Stephano Haule, wakati alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano huo na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUIAHSSO), Stephano Haule pamoja na viongozi wengine wa Serikali hiyo, Dar es Salaam leo.
 Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUIAHSSO), Stephano Haule (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuomba kurejeshwa kwa ada ya zamani kwa wanafunzi wa Cheti na Diploma wa chuo hicho, kinachoendeshwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Kulia ni Waziri Mkuu wa MUIAHSSO, Bosco Sombela na kushoto ni Makamu wa Rais wa MUIAHSSO, James Yohana.
 Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua habari zilizokuwa zikitolewa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUIAHSSO), Stephano Haule, wakati alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua habari zilizokuwa zikitolewa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUIAHSSO), Stephano Haule, wakati alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo.

AWALI YA YOTE TUNAPENDA KUTAMBUA UWEPO WENU,NA KUTOA SHUKRANI ZA DHATI KWA MWITIKIO WENU WA KUJA KUTUSIKILIZA,

PIA TUNATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA MKURUGENZI WA IDARA YA MAELEZO KWA KUTUPA KIBALI CHA KUFANYA  MKUTANO HUU WA LEO KATIKA UKUMBI HUU.PAMOJA NA WAFANYAKAZI WOTE WA IDARA HII YA MAELEZO.

UTANGULIZI

Tunatoa pongezi kwa wanataaluma  wote wa habari Tanzania kufanikisha kwa kiasi kikubwa kuibua na kuleta suluhisho kwa changamoto mbali mbali zinazolikumba Taifa letu.Pamoja na magumu mnayokumbana nayo bado dhamira yenu ya kulikomboa Taifa Inasonga mbele.Ninawapongeza sana.

Tumekuja leo hii kwa lengo kuu moja mtusaidie kufikisha  Kwa haraka zaidi hatari hii kwa Wadau muhimu  waliopo katika mamlaka mbali mbali husika,

(a)    Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
(b)   Wabunge wote wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
(c)    Wizara ya afya na ustawi wa jamii
(d)   Watanzania wote wajue hatima ya nchi yao kwani ndio wanaowachagua wawakilishi wao kwenda kutetea haki zao katika chombo muhimu cha Bunge.
(e)   N.k
Serikali ya wanafunzi kupitia Rais wake iliandika nyaraka za barua kadhaa kutoa tahadhali hii,lakini hadi sasa zimebakia siku chache tu Kwa Bajeti ya Wizara ya Afya kusomwa Bungeni,ahadi tu zimesalia tutawatumia majibu kwa njia ya barua.

HITIMISHO
Ni hatari kubwa kuona vyombo na mamlaka muhimu nchini zikifanya mzahaa na Maisha ya Watanzani.

Tunatambua wazi “hakuna haki inayoweza kuja kama zawadi”

Hivyo Serikali ya wanafunzi (MUIAHSSO) ,wanafunzi ,ikishirikiana na vyuo vyote vya afya Nchini husika na janga hili la kitaifa na Wananchi wote wa Tanzania,endapo Muhimili huu Muhimu wa Bunge utashindwa kuleta suluhisho wakati Bajeti ya Wizara Ya Afya ikipitishwa na kuacha Watanzania katika hatari hii.

Tutatambua wazi kwamba hata wawakilishi wetu tuliowapigia kura wakatutetee bungeni wametugeuka na kuamua kuisaliti Nchi Yetu na kulipeleka Taifa katika giza nene.

Hivyo  Watanzania katika hili hatutaweza kuvumilia hata kidogo hatua Muhimu zitachukuliwa ikiwamo:-
(A)   Maandamano ya amani kuomba Serikali Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Ijihuzuru,Endapo haitakuwa na suluhisho la hatari hii.
(B)   Wabunge wote wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wajihuzuru, Endapo watashindwa kuziwajibisha mamlaka husika.

Narejea kauli za Baba wa Taifa Letu Mw.J.K Nyerere “Endapo mtu yeyote hana uchungu na umasikini  tulionao hatufai hata kidogo” Wale wanaoungalia utajiri wao hatuna budi kuwang’oa kwa gharama yoyote ile kwa ukombozi wa taifa letu



MUHIMBILI UNIVERSITY
INSTITUTE OF ALLIED HEALTH SCIENCES STUDENTS’ ORGANIZATION
(MUIAHSSO)
                                                                      P.O.BOX 65005, DAR ES SALAA M.


KWA NIABA YA WATANZANIA WOTE
 



20/01/2014.

Kumb.Na.MUIAHSSO/EXCOM/TANZANIA./VOL.1

KATIBU MKUU,
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII,
S.L.P 9083.
DAR ES SALAAM.
Ndugu,

YAH:HALI YA HATARI KWA WATANZANIA WA KIPATO CHA CHINI KUKOSA KABISA FURSA                YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA AFYA KATIKA NGAZI YA CHETI (CERTIFICATE) NA STASHAHADA (DIPLOMA)

Rejea kichwa hapo juu,

 Kuna hatari kubwa ya watanzania wengi wa kipato cha chini kushindwa kujiunga na mafunzo ya fani za afya katika ngazi ya Cheti (certificate) na stashahada (diploma) kutokana na ongezeko kubwa la gharama za uchangiaji katika vyuo vya mafunzo ulioanza kwa kasi katika mwaka wa masomo wa 2012/2013.

Rejea  barua ya kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Afya  yenye Kumb.Na. JC.166/235/01‘A’/210 aliowaandikia wakuu wa vyuo vya afya  Tanzania Bara, Tarehe 19 July,2012.

Nanukuu “kutokana na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa vyuo na bajeti kuwa finyu kila mwaka Wizara imefikia uamuzi wa kuongeza viwango vya gharama za uchangiaji”

Barua hii ilitoa mwanya wa michango mingi kuongezeka.Baadhi ya vyuo ongezeko lilikuwa zaidi ya asilimia 111.9 (111.9%),160.6& na vingine ongezeko   lilikuwa  zaidi ya asilimia 174.(174%).kutoka gharama za awali.

Rejea na barua nyingine ya tarehe 04/11/2013, Yenye Kumb.Na.JB 425/558/03E/27.Nanukuu “Kutokana na kuongezeka kwa gharama ya uendeshaji wa mafunzo na upungufu wa bajeti
ya serikali, Wizara imeongeza viwango vya gharama za uchangiaji”.

Mlitumia njia hii ya kuongeza gharama kwa wanafunzi ili kunusuru uendeshaji wa vyuo ni jambo jema,lakini tatizo lilikuwa ni ufinyu wa bajeti na gharama za uendeshaji kuongezeka na matokeo yake bajeti inazidi kuwa finyu kila mwaka na gharama za uendeshaji zinazidi kuongezeka kila mwaka,hali inayozidi kumbebesha gunia la misumari mtanzania wa hali ya chini asiyeweza kumudu gharama hizi kushindwa kupata haki yake ya msingi ya kupata elimu ili aje alitumikie taifa lake.

Naiomba wizara ifikiri zaidi. Utatuzi wa tatizo la gharama kwa kuongeza gharama kubwa kwa wanafunzi itapelekea kukosa wataalamu wazuri ambao wanashindwa kujiunga na mafunzo kwa kukosa pesa.Na kama pesa itazidi kuwa ni kigezo cha kupata elimu tutambue wazi siku za usoni  tutakuwa na upungufu mkubwa  wa wafanyakazi  wa afya vijijini.

Mnatambua wazi utendaji na umuhimu wa wataalamu hawa wa afya (both certificate and diploma).Katika kuokoa maisha ya watanzania.

Hivyo naishauri wizara itafute mbinu nyingine mbadala ili kunusuru janga hili.
a)      Kupitia upya vigezo vilivyotumika kupandisha gharama ukilinganisha na kipato halisi cha mtanzania.(kipato cha mzazi au mlezi)
b)     Wizara ikishirikiana na mamlaka husika uanzishwe mfumo wa wanafunzi kupata mkopo kutoka Bodi ya mikopo kama ilivyo kwa wanafunzi wa Shahada endapo hoja ya kuwapunguzia watanzania gharama za uchangiaji inapata kigugumizi.
c)      Kurudisha vyuo vyote fya wizara ya afya kuendeshwa na serikali (Wizara) kwa maslahi ya watanzania wote.kuruhusu kwa baadhi ya vyuo kujiendesha ni kuwaumiza watanzania.
d)     Kuvunja mifumo yote inayopelekea mali za umma kutumika kwa maslahi binafsi pasina kuwafikia walengwa.
Tupo tayari  wakati wowote  tutakapohitajika kushirikiana na wizara  kutafuta suluhu ya kudumu itakayotoa matumaini mapya kwa Watanzania juu ya hoja hii.Kwa ustawi wa taifa na afya za Watanzania.

Waraka huu hauna lengo lolote la kulaumu mamlaka yoyote,ni kwa nia njema ya kutafuta suluhu ya hoja hii kwani ongezeko hilo lilikuwa ni kwa nia njema ya kuendesha vyuo.Kwa bahati mbaya hali halisi ya maisha ya watanzania ni changamoto ngumu sana kwao kumudu gharama hizo.Hivyo serikali ina kila sababu ya kuhakikisha wananchi wake wanapata elimu kwa kutumia rasilimali tulizonazo nchini.
Wako katika ujenzi wa taifa
Stephano Haule
Rais wa Serikali ya wanafunzi(MUIAHSSO) .
Simu namba:0715695619


INSTITUTE OF ALLIED HEALTH SCIENCES STUDENTS’ ORGANIZATION
(MUIAHSSO)
                                                                      P.O.BOX 65005, DAR ES SALAA M.


KWA NIABA YA WATANZANIA WOTE
 



20/01/2014.

Kumb.Na.MUIAHSSO/EXCOM/TANZANIA./VOL.1

SPIKA WA BUNGE,
BUNGE  LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
S.L.P 941,
DODOMA.

Ndugu,
YAH:HALI YA HATARI KWA WATANZANIA WA KIPATO CHA CHINI KUKOSA KABISA FURSA                YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA AFYA KATIKA NGAZI YA CHETI (CERTIFICATE) NA STASHAHADA (DIPLOMA)

Husika na kichwa hapo juu.

Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kutokana na hatari hii kubwa inayohatarisha hatima ya watanzania walio wengi kukosa fursa hii kwa kigezo cha kukosa pesa.

Tunakuomba kupitia Bunge lako tukufu.

Rejea kiambatanisho cha baru barua ya kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Afya  yenye Kumb.Na. JC.166/235/01‘A’/210 aliowaandikia wakuu wa vyuo vya afya  Tanzania Bara, Tarehe 19 July,2012.


Nanukuu “kutokana na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa vyuo {ngazi ya CHETI(CERTIFICATE) NA STASHAHADA (DIPLOMA)} na bajeti kuwa finyu kila mwaka Wizara imefikia uamuzi wa kuongeza viwango vya gharama za uchangiaji”

Rejea kiambatanisho cha waraka mwingine kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii wa tarehe 04/11/2013, Kumb.Na JB 425/558/03E/27.Nanukuu “Kutokana na kuongezeka kwa gharama ya uendeshaji wa mafunzo na upungufu wa bajeti
yaserikali, Wizara imeongeza viwango vya gharama za uchangiaji”.

Naamini Bunge lako tukufu linatambua hali halisi ya kipato cha Mtanzania.Na ni wazi kwamba watanzania walio wengi wanaishi vijijini katika maisha duni sana.Fikiria kama kulipa tu ada ya sekondari ameshindwa atapata wapi uwezo wa kujilipia laki nane,laki tisa au milioni? Na dalili zinazoonekana hali inazidi kuwa mbaya zaidi kila mwaka.

Rejea kiambatanisho Na.10.cha mfano hai wa baadhi ya chuo kimojawapo unaoonesha wazi ni jinzi gani waraka huu ulivyopelekea maumivu makali kwa watanzania. Kutoka (307,000Tshs hadi kufikia 842,400Tshs) Haya yalikuwa ni mabadiliko ya ndani ya mwaka mmjo tu,na tunakoelekea hali inazidi kuwa mbaya zaidi. Mpaka sasa tayari kunaongezeko jingine tayari na hali inazidi kuwa mbaya kwa watanzania. Bunge lako tukufu linatambua wazi hali halisi ya kipato cha mtanzania.Nimetoa kielelezo hiki ili muone wazi kama kuna usalama wowote kwa mtanzania wa kipato cha chini.

Baba wa Taifa Mwalimu J.K NYERERE wakati ule anatoa elimu bure haikumaanisha kwamba hawakuwepo watanzania wenye uwezo wa kulipia watoto wao ada za shule hapana.Ila alitambua kuwa kuna kundi kubwa la Watanzania hawataweza kulipa gharama hizo.Akaona iko sababu ya kuwekeza katika elimu.

Mheshimiwa Spika, Taifa lolote ambalo litashindwa kusomesha wananchi wake,litashindwa kuwekeza katika elimu,litabinafusisha elimu.Huo ndio utakuwa mwisho wa taifa hilo kuonekana katika ramani ya Dunia.

Mheshimiwa spika, ninakuomba sana kupitia Bunge lako tukufu,kuzuia maongezeko holela ya gharama za mafunzo katika vyuo vyote vya afya Tanzania na kutangaza rasmi mpango madhubuti wa serikali kupitia bunge lako tukufu hatima ya kuwaokoa watanzania katika mashua hii itakayozamisha wanyonge wengi

Mheshimiwa spika, Mwalimu J.K Nyerere Baba wa Taifa letu alisema maneno haya “HAKUNA KULA MBEGU WAJINGA WANAKULA MBEGU” kwa ukombozi wa Tanzania dhidi ya maadui wakuu watatu (UJINGA,UMASIKINI Na MARADHI) njia pekee ni kupanda MBEGU katika elimu,mavuno yake yataleta faraja kubwa katika taifa letu.

Mheshimiwa spika Mwalimu alisema “KWA WENYE NGUVU KUUNGANA KWAO NI UPUUZI”Hawataki kabisa kusikia wanyonge wakiungana kwasababu itakuwa ndio mwisho wao, na akasema maneno haya ”WAKATI WENYE NGUVU WANAUNGANA KUWAKANDAMIZA
WANYONGE, WANYONGE WANAGOMA KUUNGANA”

Mheshimiwa spika,wapo watu wachache ambao hawataona umuhimu wa tahadhari hii hata kidogo na kutafuta namna ya kuzifisha harakati hizi kwa makusudi kwa kuwa wana maslahi binafsi.Wapo waliojilimbikizia mali,wanaoibia umma wanatambua kwamba kama wataruhusu mwanya huu kupenya na watu wenye uchungu na nchi yao wakapata elimu ya kutosha watageuka kuwa mwiba kwa maovu yao.


Mheshimiwa spika,tunaomba katika Bunge lijalo mjadili hoja hii kwa umakini ili kuleta ahuweni kwa watanzania kwani wanaoumia si wanafunzi tu bali pia wazazi na walezi ambao wanategemea sana kutetewa na muhimili huu muhimu.
Ikishindikana kupunguza gharama hizo  basi ni wakati mwafaka kuingiza wanafunzi wa mafunzo haya katika mfumo wa kulipiwa na  Bodi ya mikopo.Kama ilivyo kwa elimu ya juu (shahada)

Mheshimiwa spika naishauri serikali kupitia bunge lako tukufu itoe miongozo itakayodhibiti upandaji wa gharama katika vyuo vya umma kwa kushirikisha wadau wote pamoja na wanafunzi.Wanafunzi wakishirikishwa vema katika mazingira ya uwazi na ukweli italiwezesha taifa kuokoa mabilioni ya pesa ya serikali yanayopotea kupitia watumishi wa umma wasiokuwa waadilifu.

MADHARA KWA TAIFA
a)      Kukithiri kwa vitendo vya kihalifu (rushwa,ujambazi,uuzaji na utumiaji madawa ya kulevya)
b)     Inatengeneza matabaka makubwa kwa aliyekuanacho na asiyekuanacho.
c)      Itapelekea miaka michache ijayo taifa kutotawalika kutokana na chuki itakayoibuka miongoni mwa matabaka (VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE)
d)     Kukosekana kwa uadilifu kwa watumishi wa umma.Mshahara anaoupata mzazi au mlezi hautoshelezi kumpeleka shule mtoto hivyo atalazimika kutumia nafasi aliyonayo kinyume na maadili kujiongezea pesa ili aweze kusomesha watoto.Kupitia Bunge lako tukufu mnatambua  hali halisi ya  maisha na kipato cha wazazi na walezi.
e)      Upungufu mkubwa wa wataalamu wa afya waadilifu siku za usoni.

Ni matumaini ya watanzania kuwa bunge lako tukufu litalishughulikia Hoja hii mapema sana,Tunaamini Bunge lijalo hoja hii itajadiliwa na kupata mwafaka ambao utapelekea mabadiliko makubwa  katika bajeti ijayo.

Sisi vijana wenu tunaipenda sana nchi yetu na tunaahidi kushirikiana bega kwa bega kutafuta suluhu za changamoto zinazolikumba taifa letu,nakusaidiana kutafuta namna ambayo itaijengea heshima kubwa nchi yetu kuwa kisiwa cha amani miaka yote.
Nimeambatanisha nakala ya barua niliyomwandikia Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na mamlaka zote husika.
Wako katika ujenzi wa taifa
Stephano Haule
Rais wa Serikali ya wanafunzi(MUIAHSSO) .
Simu namba:0715695619


INSTITUTE OF ALLIED HEALTH SCIENCES STUDENTS’ ORGANIZATION
(MUIAHSSO)
                                                                      P.O.BOX 65005, DAR ES SALAA M.


KWA NIABA YA WATANZANIA WOTE
 



20/01/2014.

Kumb.Na.MUIAHSSO/EXCOM/TANZANIA./VOL.1

JUKWAA LA WAHARIRI VYOMBO VYA HABARI
Ndugu,

YAH:HALI YA HATARI KWA WATANZANIA WA KIPATO CHA CHINI KUKOSA KABISA FURSA                YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA AFYA KATIKA NGAZI YA CHETI (CERTIFICATE) NA STASHAHADA (DIPLOMA)

Wahariri vyombo vya habari.

Kupitia taaluma yenu tunaomba mtusaidie kufanya tathmini vijijini, mijini, Kwa wakulima, wafanyakazi n.k.Muone hali halisi Na nini hatima ya Tanzania ya kesho katika elimu,mtusaidie kutufikishia hoja hii kwa viongozi husika na wawakilishi wetu Bungeni.Tuliokoe taifa letu la Tanzania.Miaka 50 ijayo wajukuu wetu waimbe wimbo wa “Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote……………..”kwa furaha tutakayoipanda leo kwa umoja kwa Taifa kuwekeza katika elimu

Hoja hii nimeitolea maelezo katika viambatanisho vya nakala za Barua kwa Katibu MKuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii na nakala ya Barua niliyomwandikia Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania.
Wako  katika ujenzi wa taifa
Stephano Haule
Rais wa Serikali ya wanafunzi(MUIAHSSO) .
Simu namba:0715695619


INSTITUTE OF ALLIED HEALTH SCIENCES STUDENTS’ ORGANIZATION
(MUIAHSSO)
                                                                      P.O.BOX 65005, DAR ES SALAA M.


KWA NIABA YA WATANZANIA WOTE
 



20/01/2014.

Kumb.Na.MUIAHSSO/EXCOM/TANZANIA./VOL.1

MWEYEKITI,
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA,
Box 2643
DAR ES SALAAM.

Ndugu,
YAH:HALI YA HATARI KWA WATANZANIA WA KIPATO CHA CHINI KUKOSA KABISA FURSA                YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA AFYA KATIKA NGAZI YA CHETI (CERTIFICATE) NA STASHAHADA (DIPLOMA)

Nanatambua mchango wenu katika kulinda na kutetea haki za binadamu.

Nchi yetu ya Tanzania ina maadui wakuu watatu:-
a)      Ujinga
b)     Umasikini
c)      Maradhi
Tunawaomba mpitie kwa umakini madai yetu,na kutusaidia kuishauri serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ione sababu ya kuweka kipaumbele cha kuwaokoa watanzania na hawa maadui  wakuu watatu hatari ambao ikiachwa bila kushugulikiwa italiteketeza taifa

Nimeambatanisha na maelezo ya hoja hii katika nakala za barua kwa Kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na nakala ya Barua niliyomwandikia Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wenu katika utetezi wa haki za binadamu,
Stephano Haule
Rais wa serikali ya wanafunzi (MUIAHSSO)
Namba ya simu:0715695619


Kumb.Na.MUIAHSSO/EXCOM/TANZANIA./VOL.1

Nakala kwa:-
1.      WAZIRI MKUU WA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA.
2.      SPIKA WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA.
3.      WAZIRI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII.
4.                  WAZIRI KIVULI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII (KAMBI YA UPINZANI BUNGENI).
5.      KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII.
6.      MKURUGENZI WA MAFUNZO WIZARA YA AFYA.
7.      JUKWAA LA WAHARIRI VYOMBO VYA HABARI TANZANIA.
8.       MWEYEKITI TUME YA HAKI ZA BINADAMUNA UTAWA BORA.
9.                  WALEZI WA WAWAFUNZI TAASISI YA AFYA NA TIBA-CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI.

KIAMBATANISHO NAMBA 10
MFANO HAI WA MABADILIKO YALIYOTOKEA NDANI YA MWAKA MMOJA TU kwa moja ya chuo cha wizara ya afya  ikiwa ni matokeo ya barua ya kaimu katibu mkuu wizara ya afya kwa wakuu wa vyuo.2011/2012,ILIKUWA LAKI TATU NA SABA elfu tu (307,000Tshs).
Mwaka wa masomo 2012/2013,ilipanda hadi kufikia laki nane arobaini na mbili elfu na mia nne.(842,400Tshs) (for Government sponsored Students)

Ongezeko hilo lilikuwa zaidi ya asilimia mia moja sabini na nne ( more than174%)kutoka gharama za awali.

No comments:

Post a Comment