Ofisa Habari toka Wakala
wa Taifa wa Utafiti wa Vifaa vya Ujenzi na Nyumba Bora (NHBRA), Bw. Frimin
Lyakurwa akiwaeleza waandishi wa Habari
(hawapo pichani) wakati wa Mkutano uliofanyika leo Katika Ukumbi wa Idara ya
Habari (MAELEZO).
Na Mwandishi wetu
WANANCHI wamehamasishwa kutumia matofali yanayofungamana, ya udongo saruji ili kupunguza
gharama za ujenzi.
Hayo
yamesemwa na Mhandisi wa Ujenzi toka Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Vifaa vya
Ujenzi na nyumba bora (NHBRA) Bw. John Twimanye wakati wa mkutano na waandishi
wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Mhandisi
Twimanye alisema Matofali hayo yanasaidia kupunguza gharama za ujenzi kwa
asilimia 30 ukilinganisha na matofali ya kawaida ya Mchanga.
“Matofali
ya udongo saruji yanapunguza gharama za ujenzi kuanzia hatua ya awali mpaka ya
mwisho ya ujenzi, pia aina zote za udongo zinaweza
kutumika kwa utengenezaji wa matofali yanayofungamana ya udongo saruji, ila
udongo ulio bora na mzuri kutumia ni ule wenye kiasi cha mfinyanzi kati ya
asilimia kumi(10%) hadi asilimia arobaini(40%).
Aidha aliongeza kuwa ujenzi wa
kutumia matofali haya hauhitaji matumizi ya Saruji ili kuyaunganisha bali
hupangwa kwa mpangilio maalum unaowezesha kuta za jengo kushikamana kwa uimara
kutokana na matundu yaliyomo kwenye matofali hayo.
Mpaka sasa Teknolojia ya matofali
hayo imetumika katika ujenzi wa Majengo Mbalimbali kwenye Mikoa ya Morogoro,
Iringa, Manyara, Tabora na Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment