TANGAZO


Thursday, April 24, 2014

Rais Jakaya Kikwete azindua ujenzi wa jengo jipya la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam

Rais Jakaya Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kuanza ujenzi wa jengo la tatu la la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba , Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Injinia Suleiman Suleiman.
Rais Jakaya Kikwete na Balozi wa Uholanzi nchini, Frederiks wakifunua pazia kuweka jiwe la msingi ka ujenzi wa jengo la tatu la JNIA
Waziri Dk. Mwakyembe akihutubia na kueleza mikakati ya kuboresha viwanja vya ndege nchini
Rais Jakaya Kikwete akitoa maagizo ya kuhakikisha wauza dawa za kulevya wanadhibitiwa kwenye Viwanja vya Ndege na kwamba majina ya wanaojihusisha kusaidia wauza dawa hizo apelekewe ili awafukuze kazi.
Rais Jakaya Kikwete, akiangalia mfano wa jengo la abiria  linalotakiwa kuanza kujengwa Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akionesha uwanja ambapo jengo hilo la Terminal 111 kitajengwa. Kengo hilo litakuwa na uwezo wa kuajiri watu 7000 na utagharimu Sh. bilioni 520.
Rais Jakaya Kikwete na Jaap Frederiks, Balozi wa Uholanzi nchini wakipongezana. Kampuni inayojenga jengo hilo ni Bam International ya Uholanzi. Ujenzi huo utakamilika Oktoba 20, 2015.

Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza jambo na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Masaburi. (Picha zote na Kamanda Richard Mwaikenda)

No comments:

Post a Comment