TANGAZO


Sunday, April 27, 2014

Shule ya Msingi ya Buguruni Wasiosikia, Yapatiwa Mtandao wa Internet wa Satelaiti

Mfuko wa Mawasilisno kwa Wote, umeanza rasmi zoezi la utekelezaji mradi wa "School Disability Connectivity Project" wenye lengo la kuzisaidia shule za umma zenye watu wenye mahitaji maalumu, kupata vifaa vya TEHAMA na huduma za mtandao wa Internet kwa matumizi ya walimu na wanafunzi lli kujifunzia na kujiletea maendeleo.

Utekelezaji huo, umeanzia katika Shule ya Msingi ya Buguruni Wasiosikia, yenye watoto wenye mahitaji muhimu ya kutosikia, ambapo Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, kwa ushirikiano na kampuni ya mawasiliano ya Avanti Communications, ya nchini Uingereza, wamepewa computes 10 za kisasa zilizounganishwa na Mtandao wa Iterneti unaitumia mitambo ya Satelaiti.

Akizindua mpango huo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiano, Sayansi na Technolojia, Dr. John Mngodo amesema Serikali inatambua kwamba shule nyingi za watu wenye mahitaji maalum, zinadahili wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali mchini Tanzania, hivyo basi mradi huu utanufaisha jamii kubwa ya Watanzania kwa ujumla.

Dr. Mngodo, ametoa rai kwa uongozi wa Shule hiyo ya Buguruni Wasiosikia, kuvitunza na kuvihudumia  vizuri vifaa hivyo ili viweze kudumu kwa muda mrefu na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa, ili kutimiza azma ya serikali  kuwawezesha watu wenye mahitaji maalum, kuweza kujiendeleza na kujiletea maendeleoi yao na ya taifa kwa ujumla.

Ofisa Mtandaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Umma, Peter Ulanga, amesema pamoja na majukumu mengine ya Mfuko wa Mawasiliano Kwa Umma, mfuko huo pia unalo jukumu kutambua watu wenye mahitaji muualum na kuwasaidia, hivyo wakaanzisha mradi huo wa "School Disability Connectivity Project"  unaohusisha shule 25 nchini Tanzania, ambapo kila shule itapatiwa compyuta 10 za kisasa na meza zake, na kwa ushirikiano na kampuni ya Avanti Communications, kila shule itaunganishwa na mtandao wa internet kupitia satelait dish

Peter Ulanga amesema Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, umeziainisha shule 25 za umma za watu wenye mahitaji muhimu zitakazopatiwa vifaa vya TEHEMA, ila itekelezaji utafanyika kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza, itazihusisha shule kumi. zikiongozwa na Shule hiyo ya Buguruni Wasio sikia, shule nyingine ni Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Shule ya Msingi Msimbazi, Shule ya Msingi Mbuyuni, Shule ya Msingi Kisiwandui, Shule ya Mazoezi ya Kufundishia Patandi, Mpilipili Maalum, Shule ya Msingi Dumila, Shule ya Msingi Manyoni na Shule ya Mtanga Maalum

Kwa upande wake, ofisa Mtendaji Mkuu wa Avanti Communications, David Williams, amesema, kampuni yake inajisikia faraja sana, kuisaidia Tanzania kutoa fursa kwa watu wenye mahitaji maalum, kuunganishwa na mtandao wa mawasiliano ya iterneti kupitia kampuni yake na kusisitiza itaendelea kuwa tayari kushirikiana na serikali ya Tanzania, katika miradi mingine mbalimbali ya mawasiliano kupitia mfuko wa mawasiliano kwa umma!.

Nae Mkuu wa Shule hiyo ya Buguruni Wasiosikia, Winfrida Jeremiah, aliishukuru serikali, Mfuko wa mawasiliano kwa Wote na Avanti Communications na kueleza kuwa msaada huo una maana kubwa sana kwa shule yake, amesema huo ni uthibitisho kuonyesha kujali, ameahidi watavitunza vifaa hivyo na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.

No comments:

Post a Comment