TANGAZO


Tuesday, April 29, 2014

Rais wa Brazil amuunga mkono Alves


Rais wa Brazil amuunga mkono Alves kwa kula ndizi

Swala tata la ubaguzi wa rangi katika michezo limeibua mchango wa rais wa Brazil.
Rais Dilma Rousseff, amesifu kitendo cha mchezaji wa kimataifa wa Brazil, na Barcelona Dani Alves kutokana na tukio la ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya ligi kuu ya Uhispania, La Liga kati ya Barcelona na Villareal .
Mchezaji huyo wa Barcelona aliokota ndizi aliyokuwa ametupiwa na kuila kabla ya kuitupa na kuendelea na mchezo.
Bi Rousseff aliandika katika mtandao wake wa twitter kuwa Dani Alves alionyesha ujasiri wa kukabiliana na ubaguzi wa rangi katika kandanda na kuwa ni tukio la kuigwa .


Rais wa Brazil amuunga mkono Alves
Klabu ya Villarreal inasema kuwa imempiga marufuku mwanaume ambaye alitupa ndizi hiyo uwanjani na kuwa hatohudhuria mechi zote za nyumbani za klabu hiyo maishani.
Mamia ya watu na wachezaji maarufu duniani wameonyesha upendo wao kwa mchezaji huyo kwa kuweka picha zao kwenye mitandao ya kijamii wakila ndizi.
Mchezaji wa Manchester City Sergio Aguero alipachika picha akila ndizi sawa na nyota ya soka ya wanawake Marta .
Wengine ni Luiz Suarez wa Liverpool, Oscar, David Luiz na Willian wote wa Chelsea .
Rais wa Fifa sepp Blatter ameongezea sauti yake katika tukio la hivi punde akisema ni vibaya kwa dhulma hizo kuendelea katika karne hii.

No comments:

Post a Comment