Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Felista Bura na Kangi Lugora, wakizungumza jambo wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kikao cha bunge hilo mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Vita Kawawa (kulia) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ahmed Mgimwa,wakizungumza jambo kwenye viwanja vya Bunge wakati wakisubiri kuingia kwenye kikao cha bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Magreth Sitta (kushoto) na Waziri wa Sheria na Katiba, Asha Rose Migiro, wakizungumza jambo ndani ya ukumbi wa Bunge, wakati wa kikao cha kuchangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita vya Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakijadili jambo nje ya ukumbi wa Bunge, mara baada ya kikao cha kuchangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita vya Rasimu ya Pili ya Katiba, kuaghirishwa leo mchana.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mohamed Said Mohamed, akichangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita vya Rasimu ya Pili ya Katiba, katika kikao cha bunge hilo leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenist Mhagama na Kingunge Ngombale Mwiru, wakizungumza jambo wakati wa kikao cha kuchangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita vya Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Alhaji Abdallah Bulembo, akichangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita vya Rasimu ya Pili ya Katiba, wakati wa kikao cha bunge hilo leo.








No comments:
Post a Comment