TANGAZO


Saturday, April 19, 2014

Ibada ya Ijumaa Kuu katika Picha Jijini Dar es Salaam Jana

Muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front, Moses Kombe, (katikati) na wenzake wakiigiza igizo la kumbukumbu ya Kuwambwa Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa hilo Dar es Salaam jana.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowasa akiwa katika ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la KKKT la Azania Front Dar es Salaam.
Waumini wa Kanisa la Kiinjili Tanzania KKT, la Azania Front la Dar es Salaam wakiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu.
Waumini wa Kanisa la Mtakatifu Joseph wakiwa kwenye ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika jana kanisani hapo.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoriki, Mwadhama Polycap Kadinali Pengo akiubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam jana.
Waumuni wa Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa wanaubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mtoto, Vanes Mpupua akiubusu Msalaba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam.
Mmoja wa Watoto waliofika katika Kanisa la Mtakatif Josef akiubusu Msaraba wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliofanyika Dar es Salaam. (Picha zote na Philemon Solomon)

No comments:

Post a Comment