SIMBA NA YANGA ZAFUNGANA BAO 1-1 TAIFA
BAO la Simon Msuva dakika ya 86, jioni hii limeinusuru Yanga SC kulala mbele ya mahasimu wake, Simba SC baada ya kupata sare ya 1-1 katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Uwanja wa Azam Complex, Chamazi bao la Brian Umony limeipa Azam ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Ruvu.Himid Mao akiwatoka wachezaji wa JKT Ruvu leo Chamazi |
Katika mchezo huo, Simba SC ilitangulia kupata bao kupitia kwa mchezaji wake, Haroun Chanongo dakika ya 68 na kwa matokeo hayo, Azam inamaliza Ligi Kuu na pointi 62 wakati Yanga SC inamaliza na pointi 56 katika nafasi ya pili. Kwa matokeo hayo Azam FC inakuwa bingwa wasiopingika wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2013/2014. (Kwa hisani ya Bin Zubeiry Blog)
No comments:
Post a Comment