TANGAZO


Wednesday, March 12, 2014

Tume ya Uchaguzi (NEC) yafanya mkutano na CCM, Chadema kuhusu maandalizi ya uchaguzi Kalenga

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (Jaji mstaafu Damian Lubuva akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa katika mkutano wa maandalizi ya ucvhaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Iinga leo. Kutoka kulia ni Mratibu wa Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Edwin Millinga (wa pili kulia) na Mratibu wa Uchaguzi CCM Jimbo la Kalenga, Miraji Mtaturu (wa tatu kulia), Mratibu wa Uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila (kushoto) pamoja na Reginald Munisi ambaye ni mwanamikakati Chadema Makao Makuu. Uchaguzi huo unafanyika Jumapili Machi 16, mwaka huu.


 Mratibu wa Uchaguzi CCM Jimbo la Kalenga, Miraji Mtaturu (kulia) akiagana na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kalenga, Pundesiana Kisaka  baada ya kumalizika kwa mkutano ulioitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), wa kujadili maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga Iringa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi (kulia), akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa vya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Miraji Mtaturu (kushoto) na Benson Kigaila wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya kumalizika kwa mkutano ulioitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), wa kujadili maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga Iringa leo. RPC Mungi alivionya vyama hivyo kutofanya vurugu katika uchaguzi huo.
 Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid akisalimiana na viongozi wa Chadema, Wakili John Malya na Reginald Munisi.
Jaji mstaafu Lubuva akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Iringa,  ambaye ni Msimamizi wa uchaguzi mdogo Jimbo la Kalenga, Pundesiana Kisaka
Jaji mstaafu Lubuva akizungumza na viongozi wa Chadema. Kutoka kulia ni Wakili wa chama hicho, John Malya na Reginald Munisi ambaye ni Mwanamikakati wa chama hicho
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Iringa, Sifael Pyuza.
Kigaila (katikati) akibadilishana mawazo na Miraji Mtaturu wa CCM.
Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mohamed Kiboko akizungumza katika mkutano huo.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kalenga, Pundesiana Kisaka akijibu hoja katika mkutano huo.
 Kigaila wa Chadema akiuliza swali katika mkutano huo.
Mratibu wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kalenga wa CCM, Miraji Mtaturu akijenga hoja katika mkutano huo.
RPC Mungi akiviasa vyama vya siasa vya CCM na Chadema kutofanya vurugu wakati wa uchaguzi na kwamba watakaokiuka sheria na taratibu watakiona cha mtema kuni.
Msimamizi wa Uchaguzi huo, Kisaka akitoa maelekezo muhimu ya uchaguzi kwa viongozi wa CCM na Chadema.
RPC Mungi akiagana na viongozi wa Chadema, Wakili John Malya (kulia) na Kigaila. (Picha zote kwa hisani ya Kamanda Richard Mwaikenda wa Kamanda wa Matukio Blog)

No comments:

Post a Comment