Nembo ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania iliozindulia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, sambamba na Uzinduzi wa sherehe za Miaka 50 ya Muungano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Makamu wake, wa kwanza Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) na wa pili, Balozi Seif Ali Idd (wa tatu), pamoja na viongozi wengine, wakiangalia burudani iliyokuwa ikitolewa wakati wa uzinduzi huo.
Wasanii wa Kikundi cha Big Star wakitowa burudani katika hafla hiyo ya Uzinduzi wa sherehe na Nembo ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapnduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akibonyeza kitufe kuashiria kuizindua Nembo ya Miaka 50 ya Muungano, katika ukumbi wa Salama Bwawani. Kulia ni Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kushoto ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, wakishuhudia uzinduzi huo.
Viongozi wa Meza Kuu wakiwa katika hafla hiyo.
Rais wa Zanzibar, akiangalia jambo pamoja na Makamu wake, wa kwanza Maalim Seif Shariff Hamad (kulia kwake) na wa pili (kushoto kwake)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia mkutano huo wa Uzinduzi wa Nembo ya Miaka 50 ya Muungano katika ukumbi wa hotele ya Bwawani.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akizungumza katika hafla hiyo ya Uzinduzi wa sherehe za Muungano na Nembo ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud, akitoa maelezo ya hafla hii ya Uzinduzi katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
Wananchi waliohudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dkt Shein akihutubia.
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Muungano wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakichukua habari wakati wa uzinduzi huo.
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa Sherehe za miaka 50 ya Muungano, mjini Zanzibar jana.
Wananchi wakifuatilia uzinduzi huo. (Picha zote kwa hisani ya Zanzinews)
No comments:
Post a Comment