Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta akitoa neno la shukrani mara baada ya tafrija fupi maalum ya kuwapongeza, yeye pamoja na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan kwa ushindi wao huo, hapo Chinese Restaurant, Mjini Dodoma jana usiku.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Suleiman Iddi, akizungumza katika tafrija fupi maalum ya kuwapongeza Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma, Samuel Sitta na Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Moh’d Aboud Moh’d, akizungumza wakati wa tafrija hiyo ya kuwapongeza Mwenyekiti na Makamu wake kwa kuchaguliwa kuliongoza Bunge Maalum la Katiba Tanzania. Tafrija hiyo, imefanyika Dodoma Hoteli katika Mgahawa wa Kichina.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan (kushoto), akiwa pamoja na mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Suleiman Iddi katika tafrija maalum ya kuwapongeza Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, mara baada ya kuchanguliwa kuliongoza bunge hilo, linaloendelea kukutana, mjini Dodoma.
Washiriki wa Tafrija hiyo fupi ya kupongezwa kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, John Samuel Sitta na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan, iliyofanyika katika Mkahawa wa China uliomo ndani ya Dodoma Hoteli. (Picha zote na Hassan Issa -OMPR)
No comments:
Post a Comment