Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana (kushoto) na Naibu wake Bara, Mwigulu Nchemba, wakimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia chama hicho, Godfrey Mgimwa, kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za lala salama, uliofanyika leo jioni katika kijiji cha Magulilwa, Kata ya Magulilwa, Iringa Vijijini.
Kinana amewataka wakazi wa Kalenga kumpigia kura za kutosha na hatimaye kuibuka mshindi kwa maendeleo ya jimbo hilo, hapo kesho (Jumapili), ambapo uchaguzi utanfanyika.
Uchaguzi unafanyika ndani ya jimbo hilo, kuziba nafasi ya aliyekuwa Mbunge wake kwa tiketi ya CCM, marehemu William Mgimwa kufariki dunia.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Magulilwa mapema leo jioni, wakati wa mkutano wa kampeni za lala salama, alipokuwa akimnadi mgombea Ubunge kupitia chama hicho, Godfreya Mgimwa kwa wananchi.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM, Godfrey Mgimwa akijinadi kwa wakazi wa kijiji cha Magulilwa, Kata ya Magulilwa, Iringa Vijijini, wakati wa mkutano wa kampeni za lala salama, amapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika kesho Jumapili, Machi 16.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mwigulu Nchemba akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia chama hicho, Godfrey Mgimwa, kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za lala salama, uliofanyika leo jioni katika Kijiji cha Magulilwa Kata ya Magulilwa, Iringa Vijijini.
Wananchi wa kijiji cha Magulilwa wakishangilia jambo katika mkutano huo leo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Kinana (kulia), kabla ya mkutano wa kampeni kuanza jioni ya leo katika kijiji cha Magulilwa, Kata ya Magulilwa, Iringa Vijijini.
Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Magulilwa akisoma moja ya gazeti la kila siku wakati mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi, ukiendelea jioni ya leo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akifarijiana na Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugora mara baada ya mkutano wa kampeni kumalizika jioni ya leo.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe, akiagana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana (kulia), mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara wa Kampeni kwa ajili ya kumnadi mgombea wa chama hicho, Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa, uliofanyika jioni ya leo kwenye Kijiji cha Magulilwa, Iringa Vijijini. Pichani katikati ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugora akisikiliza.
No comments:
Post a Comment