TANGAZO


Thursday, February 6, 2014

Waziri Kabaka azindua Baraza la Wafanyakazi SSRA

Mwakilishi wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Athuman Juma, akisoma risala ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo, wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi, lililozinduliwa naWaziri wa Kazi na Ajira, Gaudetia Kabaka, Hoteli ya Millenium Sea Breeze, Bagamoyo, mkoani Pwani leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka, akisoma hotuba yake na kisha kumkaribisha Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa SSRA, Bagamoyo leo.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akifunua pazi ili kuzindua Baraza la Wafanyakazi wa SSRA, Bagamoyo leo. Anayepiga makofi ni Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji, Sarah Kibonde Mkataba wa Huduma kwa Wateja, wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka.

Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, akimkabidhi Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, Mkataba wa Baraza la Wafanyakazi wa SSRA. Kulia anayepiga makofi ni Mkurugenzi wa Utumishi na Utawa wa wizara hiyo, Noah Mwaikuka.
Baadhi ya wafanyakazi wa SSRA, wakiwa katika mkutano wa uzinduzi huo, Bagamoyo, mkoani Pwani leo. 
Baadhi ya wafanyakazi wa SSRA, wakiwa katika mkutano wa uzinduzi huo, Bagamoyo, mkoani Pwani leo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kulizindua baraza hilo leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi huo leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka.
Mgeni rasmi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akiwa na na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, Wakurugenzi wa na wafanyakazi wa SSRA, pamoja na wageni waalikwa, mara baada ya uzinduzi huo.
Mgeni rasmi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akiwa na na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, baadhi ya Wakurugenzi na wageni waalikwa, wakiwa katika picha ya pamoja. Nyuma ni wafanyakazi wa Mradi wa Core Business Application (CBA).
Mgeni rasmi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akiwa na na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, baadhi ya Wakurugenzi na wageni waalikwa, wakiwa katika picha ya pamoja. Nyuma ni washindi wa tuzo mbalimbali wa SSRA.
Mgeni rasmi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akiwa na na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, wageni waalikwa, wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali vya SSRA.
Mgeni rasmi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, wageni waalikwa, wakurugenzi Lightness Mauki (kushoto) na Sarah Kibonde (kulia) wakiwa na Afisa Uhusiano wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji cha SSRA. Gaudiosa Mahundi (nyuma), wakati wa uzinduzi huo.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, mara baada ya kulizindua baraza hilo.

No comments:

Post a Comment