TANGAZO


Thursday, February 13, 2014

Rais wa Zanzibar Dk. Shein afunga mkutano wa Maridhiano kuelekea Katiba mpya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi alipowasili katika Hoteli ya Whitesand jijini Dar es Salaam,kuufunga mkutano wa siku mbili wa  Tafakuri na maridhiano katika  kuelekea Katiba mpya ya Tanzania leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiashiria jambo wakati wa akiufunga mkutano wa Tafakuri na maridhiano  katika kuelekea Katiba mpya ya Tanzania katika ukumbi wa White sand jijini  Dar es Salaam,uliowashirikisha wanasiasa,Mashirika ya Kijamii na Viongozi wa Dini mbali mbali nchini.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa siku mbili  kuhusu tafakuri na maridhiano katika kuelekea Katiba mpya ya Tanzania wakimsikiliza Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiufunga mkutano  uliowashirikisha watu mbali mbali wakiwemo  Wanasiasa,Viongozi wa Dini na Mashirika  ya Kijamii Nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akifuatana na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia  Tanzania pia Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Joseph Mbatia  baada ya kuufunga mkutano wa siku mbili wa Tafakuri na Maridhiano katika kuelekea Katiba mpya ya Tanzania,Ukumbi wa Whitesand Jijini Dar es Salaam leo jioni. (Picha zote na Ramadhan Othman Ikulu) 

No comments:

Post a Comment