Baadhi ya pikipiki maarufu kama bodaboda zikiwa tayari kutolewa kwa washindi wa promosheni ya Timka na bodaboda inayoesndeshwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania mara baada ya droo iliyochezeshwa katika ofisi za kampuni hiyo Bukoba mjini. Mpaka sasa jumla ya pikipiki 315 na jumla ya sh. 211 tayari zimetolewa hadi sasa, kushiriki na kushinda wateja wanatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.
Meneja wa Vodacom Bukoba, Yusuph Mnga'gi akimkabidhi funguo Rashid Kagombora, mfanyabiashara wa Wilaya ya Muleba baada ya kushinda pikipiki katika shindano la Timka na Boda boda baada ya droo iliyochezeshwa katika ofisi za kampuni hiyo Bukoba mjini. Mpaka sasa jumla ya pikipiki 315 na jumla ya sh. 211 tayari zimetolewa hadi sasa, kushiriki na kushinda wateja wanatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.
Meneja wa Vodacom Bukoba, Yusuph Mnga'gi akimkabidhi funguo, Arnod Kaisi wakala wa forodha mpaka wa Mutukula Wilayani Missenyi baada ya kushinda pikipiki katika shindano la Timka na Boda boda baada ya droo iliyochezeshwa katika ofisi za kampuni hiyo, Bukoba mjini. Mpaka sasa jumla ya pikipiki 315 na jumla ya sh. 211 tayari zimetolewa hadi sasa, kushiriki na kushinda wateja wanatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.
*Wakazi wa Kagera wakabidhiwa Pikipiki zao.
*Mfanyabiashara wa Muleba na wakala wa forodha ni miongoni mwa washindi.
Na Mwandishi wetu, Kagera
ZIKIWA zimebakia siku chache kabla ya kuisha kwa promosheni ya Timka na bodaboda inayoendeshwa na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania imeshuhudia wakazi wa Kagera wakikabidhiwa pikipiki zao zoezi liliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo mkoani humo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi bodaboda hizo Meneja wa Vodacom Bukoba, Yusuph Mnga'gi amesema kuwa wakati shindano hilo likielekea ukingoni kampuni yao imeshuhudia mafanikio makubwa hasa mikoani ambapo usafiri ni changamoto kubwa.
“Mpaka sasa tumetoa jumla ya pikipiki 315 pamoja na sh. Milioni 211, Zawadi hizi zimekuwa faraja ya kipekee kwa wakazi wa mkoa wa Kagera ambao wengi wanajishughulisha na shughuli za kilimo biashara ambazo zinahitaji usafiri wa haraka ili kuongeza uzalishaji, ni imani yangu kuwa bodaboda tunazozitoa leo zitakuwa msaada mkubwa kwao kwani sasa itawachukua muda mfupi tu kusafirisha mazao yao kutoka shambani mpaka sokoni.” Alisema Bw. Mang’agi
Meneja Masoko huyo aliongezea kuwa kampuni yao imekuwa mstari wa mbele kwa kuwa wabunifu wa huduma na bidhaa ambazo sio tu zitawanufaisha kimawasiliano bali pia kuwainua kiuchumi na kufanya maisha kuwa nafuu.
“Kupitia promosheni hii wateja wetu wameweza kujishindia usafiri wa bodaboda ambao ni maarufu na kutumiwa na watu wengi nchi nzima. Pia wameweza kujishindia fedha taslimu ambazo kwa kiasi kikubwa washindi wetu wametoa ushuhuda kuwa watazitumia ipasavyo kama mitaji na kukuza biashara zao ukizingatia wengi wamejiajiri katika shughuli zao bianafsi. Nawasihi watu kuendelea kucheza zaidi kwani tunakaribia tamati nabado zawadi zipo za kutosha tu.” Alimalizia Bw. Mang’agi
Naye Bw. Rashid Kagombora, mfanyabiashara wa Muleba ambaye ni moja ya washindi aliibuka kuwa mshindi wa bodaboda alibainisha kuwa usafiri wa uhakika ni nguzo muhimu katika kuendeleza biashara na pia kujenga uaminifu na mahusiano mazuri na wateja wangu pale unapowafikishia bidhaa kwa wakati, hivyo naweza sema usafiri huu umekuja muda muafaka. Naamini mwaka huu utakuwa wa mafanikio kwangu, nawashukuru kampuni ya Vodacom kwa zawadi hii ya mwaka mpya kwangu waendelea kutujali kwa promosheni hizi ambazo zinatunufaisha wateja wetu.
Mbali na mfanyabiashara huyo, Bw. Arnold Kaisi, wakala wa forodha katika mpaka wa Mutukula wilayani Missenyi alisema, “Sina la kusema kwa kweli zaidi ya kuwashukuru Vodacom kwa pikipiki hii, nimekuwa nikipata tabu ya usafiri kutoka nyumbani mpaka kazini ukizingatia siku zingine nachelewa kurudi lakini kwa sasa nina usafiri binafsi hakuna shaka tena.” Alisema Bw. Kaisi na kuongezea
“Kwa ushindi huu nawaomba watu washiriki katika promosheni hii kwani promosheni hii ni ya kweli na si longolongo, nimekuwa nikishiriki kwa muda mrefu sasa na ningeshangaa kama shindano lingeisha bila ya kuibuka mshindi.”
Wakati promosheni hiyo ikielekea kuisha mapema mwishoni mwa mwezi huu, kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, imewataka wateja wake kushiriki kwa wingi kwa kuandika neno PROMO kwenda nambari 15544.
No comments:
Post a Comment