Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga marehemu William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Januari 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga marehemu William Mgimwa kijijini kwake Magunga Jimbo la Kalenga, Iringa, leo Januari 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe, Mama Salma Kikwete wakitoa heshima baada ya kuweka shada la maua wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga marehemu William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Januari 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Januari 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mama mzazi wa marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Januari 6, 2014.
Mama Salma Kikwete akimfariji Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mjane wa marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo januari 6,
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa mkono wa pole wananchi wa Kalenga wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Januari 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa mkono wa pole machifu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Januari 6, 2014. (Picha zote na IKULU)
Na Francis Godwin, Iringa
MAELFU ya wakazi wa Mkoa wa Iringa na baadhi ya viongozi wa Vyama vya siasa na Serikali wakiongozwa na Rais Dk. Jakaya Kikwete, wameshiriki katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kalenga na Waziri wa Fedha Dk. Wiliam Mgimwa.
Huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika salam zake za Serikali akielezea jinsi ambavyo Taifa lilivyopata pigo kubwa kufuatia kifo cha Dk. Mgimwa kutokana na mchango wake katika Baraza la Mawaziri.
Katika mazishi hayo, yaliyofanyika leo kijiji kwake Magunga Jimbo la Kalenga wananchi mbalimbali walionyesha kujipanga barabarani kutoka Manispaa ya Iringa hadi kijijini kwake huku wakiupungia mkono msafara wa rais Kikwete na baadhi yao wakilazimika kutumia usafiri wa baiskeli na pikipiki kwenda katika mazishi hayo.
Akitoa shukrani za familia kwa niaba ya familia mtoto wa marehemu Dk. Mgimwa Godfrey Mgimwa aliishukuru serikali kwa jinsi ambavyo ilivyohangaika kumuuguza baba yake na kutoa wosia mzito wa marehemu Dr Mgimwa ambao alimtaka kuufikisha kwa Rais Kikwete.
Alisema katika uhai wake kabla ya kifo chake ikiwa ni siku tano kabla Dr Mgimwa alimwita na kumtaka kufikisha shukrani zake kwa Rais Kikwete kwa kumtembelea mara mbili Hospital alipokuwa amelazwa pamoja na spika wa bunge Anne makinda.
Pia alisema kuwa alieleza dhamira yake ya kuwatumikia wana Kalenga na kusema zawadi kubwa ni msaada wa bati zaidi ya 2000 kwa wananchi hao ili kuendeleza ujenzi wa shule na vituo vya afya jimboni.
"Baba kabla ya kufa aliniachia wosia huo juu ya wana Kalenga kwa kuwashukuru kwa ushirikiano wao na kutoa bati ila alipenda kuona Kalenga inakuwa na maendeleo zaidi"
Kwa upande wake waziri Mkuu Pinda alisema kuwa serikali imepata pigo kubwa juu ya kifo hicho na kuwa bado serikali itaendelea kuwa karibu na familia ya Dk. Mgimwa na pale penye tatizo isisite kuwasiliana .
Hata hivyo Rais Kikwete hakupata kuzungumza chochote katika msiba huo zaidi ya kuweka mchanga na shada la maua pamoja na kuwapa mkono ndugu wa Dk. Mgimwa .
Spika wa Bunge Anne Makinda alisema kuwa bunge limempoteza kiongozi na mbunge aliyependa kutumia nafasi yake kwa ajili ya Taifa na kuwa kamwe mchango wake hawataacha kuukumbuka.
No comments:
Post a Comment