Taarifa kutoka Misri zinasema kesi dhidi ya kiongozi
aliyepinduliwa nchini humo, Mohammed Morsi, imeahirishwa hadi tarehe mosi mwezi
Februari.
Lakini mshitakiwa mwenza wa Morsi alisikika akisema kuwa Morsi hawezi kuhudhuria kesi isiyokuwa na uhalali wowote.
Helikopta iliyotarajiwa kumsafirisha hadi katika mji mkuu Cairo anakokabiliwa pamoja na maafisa wengine wa utawala wake na tuhuma za kuchochea mauaji ya waandamanaji mnamo mwaka 2012 alipokuwa madarakani haingeweza kufanya safari hiyo.
Awali vikosi vya usalama viliimarisha ulinzi katika mji mkuu wa Misri Cairo ,Morsi akitarajiwa kuwasili mahakamani.
Yeye na maafisa kadhaa wa serikali yake wanatuhumiwa kwa kosa la kuchochea ghasia na kuwauwa waandamanaji mwaka 2012 wakati wa utawala wake. Mashitaka hayo ni pamoja na kushirikiana na wanamgambo wa kigeni na kuvunja gereza.
Aling'olewa madarakani kwa mapinduzi mwezi julai mwaka jana na kufungwa . Alipofika mahakamani Mwezi Novemba mwaka jana bwana Morsi alisema kuwa bado yeye ni Rais na alifungwa kinyume na matakwa yake
No comments:
Post a Comment