TANGAZO


Saturday, December 28, 2013

Mjengwa azindua kitabu chake cha Mzee Madiba, Matinyi awa mgeni rasmi

Mtunzi wa kitabu cha Mzee Madiba, Mwandishi wa habari mwandamizi nchini, Maggid Mjengwa akizungumza na wageni waalikwa, waandishi wa habari pamoja na watu mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi wa kitabu chake hicho, kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mobhare Matinyi na kushoto ni Meneja wa Habari wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Midladjy Maez. Kitabu hicho kinaelezea maisha na harakati za kisiasa za aliyekuwa Rais wa Kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela, maarufu kama 'Mzee Madiba', ambaye amefariki hivi karibuni akiacha majonzi na simanzi nyingi duniani kote. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Maggid Mjengwa akizungumza katika uzinduzi wa kitabu hicho jijijni Dar es Salaam leo.
Hii hapa ni familia ya Maggid, mke na watoto, ikiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya waalikwa, wakiwa katika uzinduzi wa kitabu hicho leo, wakifurahia maelezo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa uzinduzi huo.
Maggid Mjengwa akizungumza na hadhira iliyojitokeza kwenye uzinduzi wa kitabu cha Mzee Madiba.
Maggid Mjengwa akizungumza mambo mbalimbali, ambapo aliwahimiza wananchi kuandika vitabu ili kuweka kumbukumbu mbalimbali kwa vizazi vyetu na nchi kwa jumla.
Wageni na wananchi waliohudhuria uzinduzi wakionesha nyuso za tabasamu kutokana na yaliyokuwa yakielezwa na mtuzi huyo.
Maggid Mjengwa akielezea jambo.
Maggid Mjengwa akikazia jambo kwa jamii.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kitabu cha Mzee Madiba, Mhariri Mkuu wa zamani wa Gazeti la Majira, Mobhare Matinyi, akizungumza kabla ya kukizindua kitabu hicho, jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mtunzi wa kitabu cha Mzee Madiba, Mwandishi wa habari mwandamizi nchini, Maggid Mjengwa na kushoto ni Meneja wa Habari wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Midladjy Maez.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kitabu cha Mzee Madiba, Mhariri Mkuu wa zamani wa Gazeti la Majira, Mobhare Matinyi, akikata utepe ili kukizindua rasmi kitabu cha Mzee Madiba, jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mtunzi wa kitabu hicho, Mwandishi wa habari mwandamizi nchini, Maggid Mjengwa na kushoto ni Meneja wa Habari wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Midladjy Maez.
Mwandishi wa habari mwandamizi nchini, Maggid Mjengwa (kushoto), ambaye ni mtunzi wa kitabu cha simulizi za Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela maarufu kama Mzee Madiba (alichokishikilia), kwa pamoja na mgeni rasmi Mhariri Mkuu wa zamani wa Gazeti la Majira, Mobhare Matinyi, wakikinyanyua kukionesha kwa wageni mbalimbali na waandishi wa habari wakati wakikizindua, Dar es Salaam leo.  
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kitabu cha Mzee Madiba, Mhariri Mkuu wa zamani wa Gazeti la Majira, Mobhare Matinyi, akikinyanyua kitabu hicho, kukionesha kwa wageni mbalimbali na waandishi wa habari wakati alipokizindua, Dar es Salaam leo.  
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kitabu cha Mzee Madiba, Mhariri Mkuu wa zamani wa Gazeti la Majira, Mobhare Matinyi, akikinyanyua kitabu hicho, kukionesha kwa wageni mbalimbali na waandishi wa habari wakati alipokizindua, Dar es Salaam leo. Pamoja naye kushoto ni Mtunzi wa kitabu hicho, Mwandishi wa habari mwandamizi nchini, Maggid Mjengwa.
Mwandishi wa habari mwandamizi nchini, Maggid Mjengwa (kushoto), ambaye ni mtunzi wa kitabu hicho na mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mhariri Mkuu wa zamani wa Gazeti la Majira, Mobhare Matinyi, wakikinyanyua kukionesha kwa wageni mbalimbali na waandishi wa habari leo.
Maggid Mjengwa (kushoto) na Mobhare Matinyi, wakikinyanyua kukionesha kwa wageni mbalimbali na waandishi wa habari leo.

Mwandishi wa habari mwandamizi nchini, Maggid Mjengwa (kushoto), ambaye ni mtunzi wa kitabu cha simulizi za Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela maarufu kama 'Mzee Madiba' (alichokishikilia), kwa pamoja na mgeni rasmi Mhariri wa zamani wa Gazeti la Majira, Mobhare Matinyi, wakikinyanyua kukionesha kwa wageni mbalimbali na waandishi wa habari wakati wakikizindua, Dar es Salaam leo. 

No comments:

Post a Comment