Mchezaji wa zamani wa timu ya Ireland kaskazini na mlinzi wa
zamani wa Arsenal Pat Rice amefikishwa hospitalini baada ya kugundulika kuwa na
ugonjwa wa Saratani.
Taarifa ya klabu ya Arsenal imethibitisha kuwa Pat yu hospitali akipata matibabu na kumtumia salamu za pole na kumtakia heri apone haraka.
Rice aliichezea Gunners kwa kipindi cha zaidi ya misimu 14 baada ya kujiunga na timu ya vijana, ambapo timu yake ilichukua ubingwa wa Kombe la Ligi na FA mara mbili ,mwaka 1971, pia alikuwa nahodha wa Timu hiyo ambayo ilipata mafanikio makubwa kwenye michuano ya FA mwaka 1979.
Wenger amesifu jitihada na kazi ya Rice ambaye alikua akifanya nae kazi mpaka alipostaafu mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment