TANGAZO


Wednesday, November 27, 2013

Katibu Mkuu wa CCM, Abdurahaman Kinana atangaza kiama cha warasimu na mangimeza

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiongoza msafara kwenye migomba akitokea kufanya mkutano na Balozi James Mbasi wa Shina namba 2 la CCM Butonga, Kata ya Ikuti, wilayani Rungwe  akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama hicho na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata ilani ya uchaguzi ya CCM.Katika mikutano mbalimbali aliyoifanya wilayani humo leo Kinana alisema kuwa chama kitaanzisha mfumo wa kuwabana viongozi warasimu na mamangimeza wanaowanyima haki za msingi wananchi. (Picha zote na Richard Mwaikenda)


Kinana akizungumza katika mkutano uliofanyika nyumbani kwa Balozi  James Mbasi wa Shina namba 2 la CCM Butonga, Kata ya Ikuti, wilayani Rungwe  akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama hicho na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata ilani ya uchaguzi ya CCM.
Kinana akipanga matofali alipokuwa akizindua ujenzi wa nyumba ya mwalimu ya Shule Sekondari Ikuti, wilayani Rungwe
Wasanii wakitumbuiza kwa ngoma ya asili ya kabila la wanyakyusa ya  ing'oma  katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Ikuti.Rungwe.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Ikuti.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi akihutubia katika mkutano huo.
 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa (CCM) akihutubia katika mkutano huo.
Ndugu Kinana akihutubia katika katika mkutano huo uliofanyika katika Kata ya Ikuti, wilayani Rungwe leo.
Mbunge wa Jimbo la Rungwe Magharibi, Profesa  David Mwakyusa akielezea kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo hilo, wakati wa mkutano huo wa hadhara.

No comments:

Post a Comment