TANGAZO


Friday, October 18, 2013

Waziri Kombani aipongeza timu ya UTUMISHI kunyakua ushindi wa Pili michuano ya SHIMIWI iliyofanyika Mjini Dodoma mwezi uliopita

Watumishi na viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi Celina Kombani (Mb), wakati wa hafla fupi ya kuipongeza timu ya mpira wa Pete ya Utumishi iliyofanyika ofisini hapo mapema leo. (Picha zote na Happiness Shayo)
Baadhi ya watumishi na viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi Celina Kombani (Mb), wakati wa hafla fupi ya kuipongeza timu ya mpira wa Pete ya Utumishi iliyofanyika ofisini hapo mapema leo.
Mwenyekiti wa Klabu ya michezo ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Lumuli Mtaki akisoma ripoti kuhusu klabu yake ya Utumishi wakati wa hafla fupi ya kuipongeza timu ya mpira wa Pete ya Utumishi, iliyofanyika ofisini hapo mapema leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani (Mb), akiongea ofisini kwake katika hafla fupi ya kuipongeza  timu ya mpira wa Pete ya Utumishi mapema leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani (Mb), akiongea ofisini kwake katika hafla hiyo, fupi ya kuipongeza timu ya mpira wa Pete ya wizara yake baada ya kufanikiwa kunyakua ushindi wa pili katika michuano ya SHIMIWI, iliyofanyika mjini Dodoma mwezi uliopita.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na timu ya mpira wa Pete ya Utumishi mara baada ya hafla fupi ya kuipongeza, iliyofanyika ofisini kwake mapema leo. Wengine pichani mstari mbele ni Kapteni wa timu hiyo, Elizabeth Fussi (mwenye kikombe), Naibu Katibu Mkuu Utumishi, Bw. HAB Mkwizu, kushoto ni Mwalimu wa timu, Mathew Kambona na kulia ni Katibu Mkuu Utumishi, George Yambesi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani, akikabidhiwa kikombe na Kapteni wa Timu ya Mpira wa Pete ya Utumishi, wakati wa hafla fupi ya kuipongeza timu hiyo, iliyofanyika ofisini hapo mapema leo. Wengine pichani ni Katibu Mkuu Utumishi, George Yambesi (kulia) na Naibu Katibu Mkuu, HAB Mkwizu (kushoto), wakishuhudia tukio hilo.

No comments:

Post a Comment