TANGAZO


Sunday, October 13, 2013

Waumini wafa India ktk sherehe ya kidini


Walionusurika wanawapita waliokufa katika mkanyagano kwenye daraja juu ya mto Sindh, Madhya Pradesh
Polisi nchini India wanasema watu kama 89 wamekufa kwenye mkanyagano katika sherehe ya Kihindu.
Maelfu ya waumini walivuka daraja nyembamba kufikia hekalu la Madhya Pradesh.
Baadhi ya watu walikanyagwa, wengine walizama waliporuka kutoka daraja kwenye mto uliofurika.
Afisa wa eneo hilo alisema watu wengi walijeruhiwa na waokozi wanatafuta miili mtoni.
Polisi wanasema msongamano ulianza kulipozuka tetesi kwamba daraja ilikuwa inakaribia kuporomoka.
Lakini mashirika ya habari ya huko yanasema chanzo ni polisi kuanza kutumia virungu, kudhibiti umati.
Mikanyagano kama hiyo hutokea mara kwa mara nchini India katika sherehe za kidini ambazo huwa na mtafaruku.

No comments:

Post a Comment