TANGAZO


Sunday, October 20, 2013

Simba wafanya kile kisichowezekana watoka nyuma wakiwa wameshafungwa mabao 3 na watani zao Yanga na kusawazisha mabao yote 3


Haruna Shamte wa Simba, akijaribu kumtoka Hamis Kiiza wa Yanga wakati wa mchezo huo.
Nassor Masoud 'Cholo' wa Simba (kushoto), akijaribu kumpiga chenga Frank Domayo wa Yanga, wakati timu zao zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Timu hizo zimetoka sare kwa kufungana mabao 3-3. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Golikipa wa Yanga, Ally Mustafa 'Bartez', akijaribu kuupangua mpira uliokuwa ukiwaniwa kupigwa kichwa na Nadir Haroub 'Canavaro', wa Yanga, Betram Mombeki na Amis Tambwe, wote wa Simba. 
Abdulhalim Humud wa Simba akiruka kuupiga kichwa mpira huku akifuatwa na Haruna Niyonzima wa Yanga.
Betram Mombeki wa Simba, akupiga kichwa mpira huku akizongwa na Mbuyu Twite wa Yanga.
Wachezaji wa Simba wakiingia uwanjani kwa kuanza kipindi cha pili cha mchezo huo
Betram Mombeki wa Simba, akipiga mpira kichwa huku David Luhende wa Yanga, akijaribu kumzuiya.
Kelvin Yondani wa Yanga, akijaribu kumzuiya Amis Tambwe wa Simba wakati wa mchezo huo.
Kelvin Yondani wa Yanga, akijaribu kumtoka Amis Tambwe wa Simba wakati wa mchezo huo.
Amis Tambwe wa Simba (kushoto), akipambana na Kelvin Yondani wa Yanga, wakati wa mchezo huo. 
Kelvin Yondani wa Yanga (chini), akiwa amedondoka huku Amis Amis Tambwe wa Simba akijaribu kujizuiya asimdondokee, wakati wa mchezo huo. 

Mashabiki wa Simba wakionesha kitambaa chenye kuonesha maandishi ya kumkumbuka aliyekuwa mchezaji wao, Patrick Mafisango wakati wa mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom, kati ya timu hiyo  dhidi ya Yanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Amis Tambwe wa Simba, akipambana na Hamis Kiiza wa Yanga katika mchezo huo.
Betram Mombeki akiuchukua mpira baada ya kuifungia timu yake ya Simba bao la kwanza.
Mombeki akiuokota mpira wakati Joseph Owino, alipoifungia Simba bao la pili.
Jonas Mkude na Betram Mombeki wakiurusha mpira juu kushangilia bao hilo.
Mpira ukiwa umetoka kwenye nyavu za goli baada ya Gilbert Kaze wa Simba kuifungia timu yake bao la kusawazisha dhidi ya Yanga na hivyo timu hizo kumaliza mchezo zikiwa zimefungana mabao 3-3.
Gilbert Kaze wa Simba, akishangilia na wenzake bao la kusawazisha aliloifungia timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Yanga, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Gilbert Kaze wa Simba, akishangilia na wenzake bao la kusawazisha aliloifungia timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Yanga, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Wachezaji wa Simba wakishangilia goli hilo la tatu la kusawazisha lililofungwa na Gilbert Kaze.


 Wachezaji wa Simba wakishangilia bao lao la kusawazisha.
 Wachezaji wa Simba wakishangilia bao hilo la kusawazisha.
Wachezaji wa Simba wakishangilia mbele ya jukwa la mashabiki wa Yanga baada ya kufunga bao hilo la kusawazisha.
Hadi dakika ya 85 ya mchezo huo, timu hizo zilikuwa zimeshafungana mabao 3-3 kama inavyoonekana kwenye ubao wa matangazo.
Mashabiki wa Yanga wakiwa hawaamini macho yao kwa kilichotokea baada ya Simba kutoka nyuma ikiwa imeshafungwa mabao 3 kwa bila hadi kipindi cha kwanza kinamalizika na kisha kusawazisha mabao yote.
Mashabiki wa Simba wakifurahia hali iliyotokea katika mchezo huo, baada ya timu yao kusawazisha mabao yote 3.
Wachezaji wa Yanga wakiwa wanyonge wakitoka uwanjani baada ya Simba kusawazisha mabo yote 3.
Watangazaji wa Radio Free Africa, Hassan Mvula (kushoto) na Egbert Mkoko wakiwa kazini wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wa Simba wakiwashangilia wachezaji wao wakati wa kumalizika kwa mchezo huo.
 Golikipa wa Simba, Abel Dhaira (kulia), Abdulhalim Humud na Betram Mombeki wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika mchezo huo.
Wachezaji wa Simba wakipongezana baada ya kumalizika mchezo huo.
Kocha msaidizi wa Simba Jamhuri Kiwelo, akiwalaki wachezaji wake baada ya kumalizika mchezo huo.
 Wachezaji wakitoka uwanjani.


Wachezaji wa Yanga wakitoka uwanjani wakiwa na huzuni kubwa baada ya Simba kusawazisha mabao yao, yote 3, waliyoyafunga katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

No comments:

Post a Comment