TANGAZO


Monday, October 21, 2013

Shirika la Viwango Tanzania, latoa taarifa kwa waandishi wa habari, kuhusu udhibiti wa Ubora wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi kabla ya kusafirishwa (PVoC)

Ofisa Uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Roida Andusamile, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, kuhusu ufunguaji wa Ofisi za Shirika hilo, katika maeneo ya mipakani ili kudhibiti uingizwaji wa bidhaa zilizo chini ya kiwango, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO) leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO), Frank Mvungi. (Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)

Ofisa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), David Ndibalema (kushoto), akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu mfumo wa Udhibiti wa Ubora wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi kabla ya kusafirishwa (PVoC), utakaosaidia kuondoa tatizo la bidhaa hafifu, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO) leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa shirika hilo, Roida Andusamile.

SHERIA MPYA
Imebainisha hatua kadhaa iwapo inabainika kuwepo kwa bidhaa hafifu:-

       Kuondoa bidhaa hafifu zilizopo sokoni;

       Kufuta leseni;

       Kuweka utaratibu wa marejesho;

       Kuharibu bidhaa duni au kuzirudisha zilikoagizwa;

       Kutoza faini.
MAJUKUMU NA MADHUMUNI
Majukumu makuu ya Shirika ni

       Kukuza matumizi ya viwango;

       Kuinua ubora wa bidhaa na huduma nchini ili kulinda afya na usalama wa walaji, kulinda mazingira, kupanua soko la nje kwa bidhaa zetu na kukuza uchumi;

       Kudhibiti uingiaji wa bidhaa ndani ya nchi ili kuhakikisha ni bidhaa bora tu ndizo zinaruhusiwa kuingia nchini.

UDHIBITI WA UBORA WA BIDHAA ZINAZOTOKA NJE YA NCHI KABLA YA KUSAFIRISHWA (PVoC)

Kuna mifumo ifuatayo katika ukaguzi wa bidhaa:

Destination Inspection (DI).

       Ukaguzi wa bidhaa unaofanyika baada ya sherena kufika nchini kabla ya kuingia sokoni.

 MIKAKATI ILIYOPO YA DESTINATION INSPECTION

       Ukaguzi wa bidhaa sokoni.

       Uanzishwaji wa ofisi za TBS mipakani.

       Ukaguzi wa mara kwa mara katika masoko (market surveillance).

       Udhibitishaji wa makampuni ya nje kupitia utoaji wa leseni za ubora.

       Kutambua udhibiti wa mashirika ya Viwango ya nje.

Pre-shipment Verification of Conformity to Standards(PVoC)

       Ukaguzi wa ubora wa bidhaa unaofanyika kabla ya shehena kusafirishwa.

       Mfumo wa udhibiti unaotumika kuhakiki bidhaa zinazoingizwa zinakidhi matakwa ya Viwango vya Taifa na vya Kimataifa.

MADHUMUNI NA FAIDA ZA PVoC

       Kuhakiki bidhaa zinazoingizwa nchini zinakidhi matakwa ya viwango vya Tanzania au Kimataifa kabla hazijasafirishwa.

       Kulinda afya na usalama wa watumiaji pamoja na kuzuia uchafuzi wa mazingira.

       Kuongeza ufanisi wa kuondoa shehena bandarini na kupunguza mlundikano wa shehena bandarini (trade facilitation)
       Kulinda viwanda vya ndani dhidi ya ushindani usio wa haki (unfair competition) unaosababishwa na uwepo wa bidhaa zenye ubora hafifu zilizoagizwa toka nje ya nchi.

       Kwenda sanjari na mageuzi ya teknolojia yanayofanywa na TRA na TPA, yanayolenga kuondoa mlundikano wa shehena.

       Kuzuia Tanzania isigeuzwe jalala la bidhaa zenye ubora hafifu.

UTEKELEZAJI WA PVoC

       Mnunuzi wa Tanzania  anatakiwa kuwasiliana na muuzaji wake nje ya nchi, kwa kumueleza bidhaa anayoihitaji na viwango vyake 

       Muuzaji anatakiwa kuwasiliana na wakala wa huduma za PVoC aliyepo karibu naye ili kupata utaratibu wa kufuata kabla ya kusafirisha shehena.

       Wakala wa PVoC hupima bidhaa husika na kutoa cheti cha ubora (CoC) endapo bidhaa hiyo itakidhi matakwa ya kiwango.

       Wakala wa PVoC hutuma CoC halisi (Original) kwa mnunuzi aliyeko Tanzania na nakala ya CoC hutumwa kwa muuzaji.

       Mnunuzi huwasilisha CoC halisi TBS kwa kuhakiki na TBS hutuma CoC hiyo TRA kwa njia ya kielektroniki ili kuruhusu shehena kutolewa bandarini.

       TBS inafanya ukaguzi kwa wakala wa PVoC mara moja kwa mwaka kuhakikisha kazi imefanyika kulingana na mkataba.

UZOEFU WA NCHI NYINGINE ZA KIAFRIKA

       Shirika la Viwango Kenya (KEBS) lilianza PVoC June 2005 hadi leo linaendelea kutekeleza

       Asilimia 75 ya bidhaa zinazoingia Kenya zinakidhi matakwa vya Viwango

       Kwa Afrika, PVoC inatekelezwa Nigeria, Botswana Ethiopia, Ghana, Burkina Faso na Uganda
HITIMISHO

       Mfumo wa PVoC umefanikisha lengo la kuzuia bidhaa zisizo na ubora kuingia nchini kwa asilimia 65, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na TBS mwezi Desemba, 2012, baada ya kuwahoji wasambazaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Mara na Kagera.

No comments:

Post a Comment