TANGAZO


Monday, October 21, 2013

Maadhimisho ya Wiki ya Usalama barabarani, mkoani Dodoma

Waendesha Bodaboda, mjini Dodoma wakiandamana katika maandamano ya amani yaliyoanzia Kituo cha Polisi cha Kati kuelekea Viwanja vya Barafu, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama barabarani, mjini humo jana.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, akimkabidhi cheti dereva bora, wakati wa maadhimisho hayo.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakiongoza maandamano ya Wiki ya Usalama Barabarani, yaliyofanyika jana mkoani Dodoma.
Kipima ulevi kitakachotumiwa na Polisi wa Usalama Barabarani, kuwagundua madereva wanaoendesha vyombo vya usafiri huku wakiwa wamelewa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Dodoma, Suzan Kaganda na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Ester Mgongolwa, wakienda kupokea maandamano ya maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani jana.
Pc Jerome Mbano, akimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, jinsi kipima ulevi kwa madereva kinavyofanya kazi, wakati wa maadhimisho hayo. (Picha zote na John Banda, Dodoma)

No comments:

Post a Comment