TANGAZO


Thursday, October 24, 2013

Chuo cha Serikali za Mitaa chafanya mafunzo kwa watumishi wa Serikali 4,913

*Chaongeza udahili kwa mwaka wa masomo 2013/2014
 
Ofisa Uhusiano wa Chuo cha Serikali za Mitaa, Sebera Fulgence akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu mafanikio ya Chuo hicho, ikiwa ni pamoja na kufanya mafunzo kwa Watumishi wa Serikali  wapatao 4,913, katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Rebecca Kwandu. (Picha na Eliphace Marwa-Maelezo)

Chuo cha Serikali za Mitaa, Hombolo Dodoma kimetoa mafunzo kwa Watumishi zaidi ya 4,913 toka 2009 mpaka kufikia Septemba 2013 kwa  Watendaji na Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, pia idadi ya walionufaika na mafunzo haya ni kama ifuatavyo:
a)    Wenyeviti wa Vijiji/Mitaa/Vitongoji          3,733
b)    Maafisa Watendaji wa Vijiji/Mitaa  282
c)     Maafisa Watendaji wa Kata 388
d)   Madiwani 327

e)     Wawezesha Mafunzo 52
f)      Maafisa Elimu Sekondari  48
g)    Wahudumu wa Ofisi 20

h)    Wajumbe wa ALAT 18

i)      Wakuu wa Idara 45

Pia Chuo kwa kushirikiana na Taasisi ya Forum syd ya Mwanza, tangu mwaka 2011  kimeweza kutoa mafunzo ya muda mfupi ya Uwajibikaji wa Kijamii (Social Accountability) kwa watumishi na viongozi wa ngazi zote za Serikali za Mitaa pamoja na Asasi za Kiraia, wakiwemo Wenyeviti na Maafisa Watendaji wa vijiji, Vitongoji, Mitaa na Kata, Waheshimiwa Madiwani, Wakurugenzi na wakuu wa Idara na Vitengo,  Wakuu wa Magereza, Mabenki, TAKUKURU, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na Maafisa Tarafawa Halmashauri za Wilaya za Ukerewe, Magu na Karagwe .

Mwaka 2009  Chuo cha Serikali za Mitaa kiliteuliwa na Serikali kuwa Taasisi Kiongozi ya Mafunzo (Lead Training Institution) katika kuratibu na kusimamia ubora wa mafunzo yatolewayo kwa watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Kazi hiyo kwa sasa inafanywa na Chuo kwa kushirikiana na wafadhili. Kwa sasa wafadhili ambao  ni JICA na GIZ. Aidha, Mwaka 2012 Chuo cha Serikali za Mitaa kiliteuliwa na Serikali kutoa mafunzo elekezi (Induction Courses) kwa watumishi wote wapya wanaoajiriwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Jukumu hilo ni kwa mujibu wa Waraka namba 5 wa Utumishi wa Umma wa mwaka 2012.

Aidha, Chuo kwa kushirikiana na OWM TAMISEMI, kiliendesha mafunzo ya Semina elekezi ya Makatibu Tawala wapya wa Mikoa sita (6) ya Tanzania Bara mwezi Mei 2011 na Makatibu Tawala wa Mikoa yote tarehe 4/7/2011 hadi tarehe 13/7/2011.

Mafunzo haya yamekuwa yakifanyika hapa Chuoni na Mengine kwenye Mikoa husika ya Watumishi.

Chuo cha Serikali za Mitaa ni miongoni mwa Taasisi zilizoko chini ya OWM-TAMISEMI na kilianzishwa kwa mujibu wa Sheria Na. 26 ya mwaka 1994 (Sura ya 396 toleo lililorejewa mwaka 2002). Lengo kuu la kuanzishwa kwake ni kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kutoa huduma bora zitakazowajengea wananchi uwezo wa kuimarisha utawala bora, kuondokana na umaskini na kuboresha maisha yao.
Madhumuni mahususi  ya Chuo ni kuchangia katika uwezeshaji wa mchakato mzima wa kupeleka madaraka  kwa wananchi, kujenga na kukuza utawala bora, kukuza uchumi na kuondoa umaskini  katika ngazi  mbalimbali za Serikali za Mitaa hapa nchini.
Chuo hiki kimesajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (National Council for Technical Education) ambalo ndilo lenye mamlaka ya kusimamia ubora, viwango na uendeshaji wa Vyuo vya Elimu ya juu na Ufundi visivyo Vyuo Vikuu hapa nchini.
Majukumu ya Chuo yamegawanyika katika sehemu kuu tatu:-

i)       Kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu juu ya taaluma, ujuzi, stadi na mbinu za uendeshaji wa Serikali za Mitaa kwa Viongozi na Watumishi walio katika ngazi mbalimbali za Serikali za Mitaa;

ii)     Kutoa mafunzo juu ya mabadiliko yanayohusu Serikali za Mitaa kulingana na Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa na;

iii)  Kufanya utafiti na kutoa ushauri kwa Serikali Kuu, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mashirika na watu binafsi juu ya masuala yote yanayohusu Serikali za Mitaa.

Chuo katika kutimiza lengo lake la kuwa ndicho Chuo Kiongozi cha Mafunzo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, kinaendelea na jitihada zake za kuhakikisha kuwa zinawafikia watumishi wote wa Mamlaka  za Serikali za Mitaa kupia mafunzo ya kuwajengea uwezo wao kiutendaji na kitaaluma. Pamoja na jitihada zinazofanywa na Chuo katika utoaji wa mafunzo ya muda mfupi na yale ya Muda mrefu, bado kinakabiliwa na changamoto moja kubwa kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa ni uhaba wa fedha za mafunzo kinachopelekea kutofanyika kwa mafunzo mengi kwa Watumishi  ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ambao ndio Wadau Muhimu.


UDAHILI
Chuo cha Serikali za Mitaa [The Local Government Training Institute] Hombolo , Dodoma kimedahili Wanafunzi 1603 kwa mwaka wa masomo 2013/2014. Idadi hii inajumuisha Wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na kujiunga na Astashahada (Basic Technician Certificate courses) na kidato cha sita wanaojiunga na Stashahada (Ordinaly Diploma Courses) katika fani za Uhasibu na Fedha, Uongozi na Uendeshaji katika Serikali za Mitaa, Maendeleo ya Jamii na Menejimenti ya Rasilimali Watu. Idadi hii ya wanafunzi waliodahiliwa na wale wanaoendelea na masomo inafanya  Wanafunzi wote kufikia 2,491 kwa mwaka wa masomo 2013/2014.

 

Idadi hii ni sawa na ongezeko la asilimia 96.5%  ukilinganisha na jumla  ya wanafunzi 86 waliodahiliwa katika mwaka wa masomo 2007/2008. Kimsingi Idadi ya Wanafunzi wanaojiunga na Chuo hiki imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka kuanzia mwaka wa Masomo 2007/2008, kwa sababu zifuatazo:-

a)    Kuongezeka kwa kozi kutoka kozi nne (4) za awali mpaka kozi nane(8) kwa sasa.

b)    Kuongezeka kwa Watumishi Wanataaluma na Waendeshaji kutoka 38 mwaka 2007/2008 hadi 108 mwaka 2013/2014

c)     Kuongezeka kwa miundombinu mipya ya kujifunzia na kufundishia kama ifuatavyo:-

                    (i)        Mabweni (8) yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 1,620 jumla;

                  (ii)      Madarasa (8) yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 jumla;

                 (iii)     Ofisi (8) zenye uwezo wa kuchukua zaidi ya watumishi 10;

                 (iv)     Maktaba yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 300 kwa pamoja;

                   (v)      Maabara ya kompyuta yenye uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 300 kwa pamoja;

                 (vi)     Bwalo la chakula na jiko la kisasa lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 300 kwa pamoja;

                (vii)   Nyumba za makazi ya Watumishi (15), yaani daraja A (5) na daraja B(10);

              (viii)  Ukumbi wa kutolea mihadhara namba 3 ambao una uwezo wa kubeba watu 576;

                 (ix)     Kumbi za mihadhara namba moja na namba mbili zenye uwezo wa kubeba watu 400;

Aidha, Chuo kimeanza ujenzi wa Kituo cha Afya cha kisasa kitakachogharimu kiasi cha shilingi bilioni 7.8 Lengo kubwa la ujenzi wa kituo hiki ni kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa Wagonjwa wapatao 3000 wajumuiya ya Chuo ikiwemo wanakijiji waliozunguka Chuo.

 

Chuo cha Serikali za Mitaa ni miongoni mwa Taasisi zilizoko chini ya OWM-TAMISEMI na kilianzishwa kwa mujibu wa Sheria Na. 26 ya mwaka 1994 (Sura ya 396 toleo lililorejewa mwaka 2002). Lengo kuu la kuanzishwa kwake ni kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kutoa huduma bora zitakazowajengea wananchi uwezo wa kuimarisha utawala bora, kuondokana na umaskini na kuboresha maisha yao.

Madhumuni mahususi  ya Chuo ni kuchangia katika uwezeshaji wa mchakato mzima wa kupeleka madaraka  kwa wananchi, kujenga na kukuza utawala bora, kukuza uchumi na kuondoa umaskini  katika ngazi  mbalimbali za Serikali za Mitaa hapa nchini.

Chuo hiki kimesajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (National Council for Technical Education) ambalo ndilo lenye mamlaka ya kusimamia ubora, viwango na uendeshaji wa Vyuo vya Elimu ya juu na Ufundi visivyo Vyuo Vikuu hapa nchini.

Majukumu ya Chuo yamegawanyika katika sehemu kuu tatu:-

i)       Kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu juu ya taaluma, ujuzi, stadi na mbinu za uendeshaji wa Serikali za Mitaa kwa Viongozi na Watumishi walio katika ngazi mbalimbali za Serikali za Mitaa;

ii)     Kutoa mafunzo juu ya mabadiliko yanayohusu Serikali za Mitaa kulingana na Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa na;

iii)  Kufanya utafiti na kutoa ushauri kwa Serikali Kuu, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mashirika na watu binafsi juu ya masuala yote yanayohusu Serikali za Mitaa.

Vilevile kinashirikiana na Vyuo au Taasisi nyingine katika kujiletea maendeleo ya kitaaluma na pia maendeleo kwa wananchi. Vyuo na taasisi hizo ni kama vile Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP - Dodoma), Chuo Kikuu cha Dodoma, Taasisi ya SYD-Forum (Sweden), Chuo Kikuu Mzumbe, Taasisi ya Maendeleo ya Maafisa wa Serikari za Mitaa (LOGODI - Local Government Officials Development Institute) ya Korea na Chuo cha Uongozi cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (Dar es Salaam).

Vilevile kinashirikiana na jamii iliyo karibu katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikumba  hususani suala la maji kwa wananchi walio karibu na Chuo, kuchangia madawati na ujenzi wa shule za msingi, kutoa ufadhili kwa wanafunzi wasiojiweza kifedha ili kuwawezesha kupata mafunzo yatolewayo hapa Chuoni na huduma nyingine.

Pamoja na kutekeleza majukumu tajwa hapo juu, Chuo  kinakabiliwa na changamoto mbali mbali kama vile ubovu wa barabara ya Ihumwa – Hombolo yenye urefu wa kilomita 27 ambayo haijajengwa kufikia angalau kiwango cha changarawe hali ambayo inafanya magari yanayotumia barabara hiyo kuharibika mara kwa mara hivyo kuongeza gharama za matengezo.
Ombi letu kubwa katika suala hili ni barabara hiyo kutengenezwa kwa kiwango cha lami.
Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
Chuo Cha Serikali za Mitaa, Hombolo Dodoma
24.10.2013

No comments:

Post a Comment