Mashabiki wa Yanga, wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo na Azam FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Didier Kavumbagu (kulia) wa Yanga akiwania mpira na Kipre Balou wakati wa mchezo huo.
Simon Msuva wa Yanga, akipiga krosi mbele ya Waziri Salum wa Azam FC katika mchezo huo.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la pili la timu hiyo wakati wa kipindi cha pili cha mchezo huo.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia kwa staili ya aina yake bao la pili la timu hiyo wakati wa kipindi cha pili cha mchezo huo.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia kwa staili ya aina yake bao la pili la timu hiyo, lililofungwa na Hamis Kiiza, wakati wa kipindi cha pili cha mchezo huo.
Said Morad wa Azam FC akiwa ameruka juu ya Athuman Idd wa Yanga wakati wa mchezo huo.
Athuman Idd akiwajaribu kuudhibiti mpira wa juu huku akifuatwa na Kipre Balou wa Azam FC.
Didier Kavumbagu wa Yanga, akiruka juu pamoja na Said Murad wa Azam FC (15), kuwania kuupiga kichwa mpira katika mchezo huo.
Waziri Salum wa Azam akipiga shuti mpira huku akifuatwa na Hamis Kiiza wa Yanga.
Golikipa wa Azam, Aishi Manula, akiruka juu kuudaka mpira uliokuwa umeelekezwa langoni kwake.
Hamis Kiiza wa Yanga, akikimbia na mpira huku akifuatwa na Waziri Salum wa Azam FC.
Said Murad wa Azam FC, akiondoa mpira langoni mwa timu hiyo katika mchezo huo.
Didier Kavumbagu wa Yanga akiruka sambamba na David Mwantika (12) wa Azam FC.
Said Murad wa Azama FC (kulia), akimzuiya Simon Msuva katika mchezo huo.
Hadi karibu na dakika ya 88 timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2 baada ya kuingia dakika ya 89, Azam wakafunga goli lao la 3 na la ushindi katika mchezo, kama inavyoonekana kwenye ubao wa matangazo, baada ya kukoswa koswa na wapinzani wao hao kwenye dakika ya 88 ya mchezo huo.
Simon Msuva wa Yanga akiruka juu kuuwahi mpira kuupiga kichwa huku akipambana na Waziri Salum.
Mashabiki wa Yanga wakiwa wamechanganyikiwa baada ya kufungwa bao la 3 na Azam FC kama wanavyoonekana pichani.
Erasto Nyoni wa Azam akimpongeza mfungaji wa bao
la 3 la timu hiyo, katika mchezo huo dhidi Yanga, Joseph Kimwaga, baada ya
kumalizika kwa mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam leo jioni. Azam ilishinda mabao 3-2.
No comments:
Post a Comment