TANGAZO


Sunday, September 22, 2013

Rais Shein awataka wananchi kuendeleza juhudi za kuzuiya maambukizi mapya sambamba na vita dhidi ya dawa za kulevya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mkurugenzi wa ZAPHA+ Seif Juma Abdalla,alipowasili kulizindua jengo jipya la Jumuiya Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi huko Welezo leo, (kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya ZAPHA+ Bi Hasina Hamadi. (Picha zote na Ramadhan Othman)
Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe kama isahara ya kulizindua jengo jipya la Jumuiya Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi ZAPHA+ huko Welezo leo,(katikati) Mwenyekiti wa Bodi ya ZAPHA+ Bi Hasina Hamadi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto)akimuangalia Mshauri nasaha Suluhu Ramadhan (kulia) alipokuwa akitoa huduma kwa Hapsa Rakwe,(mwenye buibui) alipokuwa akitembelea sehemu mbali mbali za   jengo jipya la Jumuiya ya Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi ZAPHA+ huko Welezo leo, baada ya kulizindua Rasmi leo.
Wanafunzi waliohudhuria katika ufunguzi wa jengo jipya la Jumuiya Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi ZAPHA+ huko Welezo leo,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa hutuba yake katika sherehe hizo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, (katikati) alipokuwa akitia saini kitabu cha wageni alipofika katika sherehe za uzinduzi wa jengo jipya la Jumuiya ya Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi ZAPHA+ huko Welezo leo,kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya Bi Hasina Hamadi.
Vijana waliofanya Igizola Unyanyapaa kwa watu wanaoishi na Virusi vinavyosababisha Ukimwi, wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la Jumuiya ya ZAPHA+ leo,wakati    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) alilizindua jengo hilo huko Welezo Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Mtoto Suhaila Mshamu, ni miongoni mwa Watoto wanaoishi katika mazingira magumu akisoma Risala kwa niaba ya watoto katika wilaya mbali mbali,wakati wa sherehe za Uzinduzi wa jengo jipya la Jumuiya ya ZAPHA+ leo,mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya Wananchi wakiwa mbele ya bango linaloptoa ujumbe”Jukumu la kuwatunza na kuwalea Watoto walio katika Mazingira Magumu ni letu Sote”,walipokuwa katika sherehe za Uzinduzi wa jengo jipya la Jumuiya ya ZAPHA+ zilizofanyika leo,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
Wazee waliofika kumliwaza Mtoto Suhaila Mshamu,wakati alipokuwa akisoma risala kwa  niaba ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu  wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la Jumuiya ya ZAPHA+leo,mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi ZAPHA+ Consolata John,alipokuwa akisoama risala ya jumuiya hiyo wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la jumuiya hiya hiyo huko Welezo Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi ZAPHA+,Bw.Khamis Mbarouk,(akinyanyua mikono juu) alipotambulishwa wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jengo jipya la jumuiya hiyo huko Welezo Mjini Unguja,mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi ZAPHA+ Consolata John,akisoma risala.
Baadhi ya Wananchi na Wanajumuiya wa Zapha +wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani)alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jengo jipya la Jumuiya ya ZAPHA+huko Welezo leo. 
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi ZAPHA+ Consolata John,alipokuwa akimkabidhi risala ya kwa niaba ya wanachama wenzake kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jengo jipya la Jumuiya hiyo huko Welezo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,alipokuwa  akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jengo jipya la Jumuiya ya ZAPHA+huko Welezo leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu,wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jengo jipya la Jumuiya wanaoishi na Virusi vya Ukimwi huko Welezo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,alipokuwa  akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jengo jipya la Jumuiya ya ZAPHA+huko Welezo leo.

Na Said Ameir, Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema jitihada za kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya ugonjwa wa UKIMWI nchini hazina budi ziende sambamba na vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vingine ambavyo ni miongoni mwa vyanzo vya ugonjwa huo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Kituo cha Jamii na Watoto huko Welezo Wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo Dk. Shein amesema imebainika kuwa maambukizi mapya ya virusi vya ugonjwa huo kwa vijana yanahusishwa na matumzi ya madawa ya kulevya.

“Katika miaka ya hivi karibuni imebainika kuwa maambukizi mapya ya UKIMWI yanawakumba zaidi vijana wanaotumia dawa za kulevya hapa nchini” Dk. Shein alieleza.

Kituo hicho kimejengwa na Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ugonjwa wa UKIMWI Zanzibar ZAPHA+ kwa msaada wa taasisi ya Stephen Lewis Foundation ya Canada ambayo ilichangia shilingi milioni 43.65 ambazo ni sawa na asilimia 40.45

Kwa hivyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali na washirika wengine katika mapambano dhidi ya maambukizi ya UKIMWI na dawa za kulevya kuiokoa jamii hasa vijana ambao ni tegemeo la taifa.

Dk. Shein amewaeleza wanachama wa ZAPHA+, wananchi na wageni waliohudhuria hafla hiyo kuwa tangu ugonjwa huo ulipogunduliwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikifanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuhakikisha Zanzibar haipati maambukizi mapya na pia kuondosha unyanyapaa dhidi ya watu walioathirika na ugonjwa huo.

“...Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikichukua hatua mbali mbali ili kuhakikisha kwamba tunakuwa na Zanzibar isiyokuwa na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI, isiyokuwa na unyanyapaa wala ubaguzi unaotokana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI” Dk. Shein alieleza.

Amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kuunda taasisi za kuratibu na kushughulikia mapambano dhidi ya ugonjwa huo, kushiriki katika kutekeleza sera, mipango, na mikakati mbalimbali kwa kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika mapambano hayo.
Kwa hiyo ametoa wito kwa wananchi kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kuzingatia utekelezaji wa mipango iliwekwa na Serikali kwa kushirikiana na sekta zisizokuwa za Serikali.

Kuhusu huduma na tiba kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ameeleza kuwa zimeendelea kuimarishwa kwa kuongeza vituo vya huduma na tiba hadi kufikia vituo kumi kutoka kituo kimoja mwaka 2005.

“...dawa za ARV zimekuwa zikipatikana katika vituo mbalimbali bila malipo...huku serikali imeimarisha huduma za uchunguzi wa maradhi ili kuongeza ufanisi katika kukabiliana na janga hili” Dk. Shein alibainisha.

Dk. Shein ameupongeza uongozi wa ZAPHA+ na wanachama wake kwa jitihada zao hadi kuweza kujenga jengo hilo ambalo litawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo. 
Akizungumzia kuendelea kupungua kwa misaada ya wafadhili kwa shughuli za UKIMWI Dk. Shein ameahidi kuwa Serikali itaendelea kutafuta namna bora ya kusaidiana na taasisi kama ZAPHA+ ili kutekeleza majukumu ya mapambano dhidi ya UKIMWI.

Hata hivyo ametoa wito kwa uongozi wa ZAPHA+ kutafuta njia za kujiongezea mapato kwa kubuni miradi ikiwemo ya kujitegemea.   

Amewataka wananchi kutumia fursa ya kuwepo kwa jumuiya hiyo kwa kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu maradhi ya UKIMWI kwa manufaa yao binafsi na pia kama sehemu ya jitihada za pamoja kupambana na maradhi hayo nchini.

Rais alitumia fursa hiyo kuwashukuru watu na taasisi mbali mbali ambazo zimekuwa zikisaidia Zanzibar katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI tangu kugundulika kwake hapa Zanzibar miaka 27 iliyopita.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna, Waziri wa Afya Juma Duni Haji,Mkuu wa Mkoa Mjini Maghribi Abdalla Mwinyi Khamis na washirika mbalimbali wanaounga mkono mapambano dhidi ya UKIMWI yakiwemo Mashirika ya Kimataifa.

No comments:

Post a Comment