TANGAZO


Tuesday, September 24, 2013

Viongozi wa maziwa makuu waafikiana



Mkutano wa viongozi wa masiwa makuu
Viongozi wa bara Afrika kutoka eneo la Maziwa Makuu wameapa kutekeleza azimio la mazungumzo ya amani kwa eneo la Mashariki mwa taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Katika mkutano uliofanyika kandakando ya vikao vya umoja wa mataifa, viongozi hao wameamua kutosaidia upande wowote na vilevile kutoa wito kwa serikali ya DRC na waasi wa M23 kusitisha vita hivyo.
Azimio hilo jipya ni ishara ya hatua muhimu kwa nchi ambayo imekumbwa na mgogoro kwa miaka mingi, hususan katika eneo la Mashariki mwa nchi, ambako maelfu wameuawa na wengine wengi kuachwa bila makao baada ya kutoroka vita.
Mary Robinson, mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa katika eneo la Maziwa makuu, aliambia waandishi wa habari baada ya kukutana na viongozi kumi kutoka eneo la Maziwa makuu, kwamba bado kuna kazi nyingi ya kufanywa kutekeleza mapendekezo hayo.
Mgogoro wa Congo unatokana na mauaji ya Kiambari yaliyofanyika Rwanda mwaka 1994 ambapo mamia ya wakimbizi wa kihutu waliohusika na mauaji hayo walikimbilia Congo, na bado wanapigania kutoka huko.
Mapigano ya sasa ni kati ya kundi la waasi la M23 na jeshi la serikali.Waasi hao walianza mashambulio mwezi uliopita kabla ya kufurushwa kutoka mji wa Goma kupitia usaidizi wa vikosi vya umoja wa mataifa.
Lakini ahadi iliyotolewa ya kila nchi kutoingilia maswala ya ndani ya nchi jirani, ni muhimu kwa sababu jamii ya kimataifa imekuwa ikituhumu Rwanda kwa kuchochea zaidi mgogoro unaokumba DRC kwa kuunga mkono waasi wa M23 na kuitumia kama ndowano ya kupora madini katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment