TANGAZO


Saturday, September 14, 2013

Vifo vya watoto vyapungua Ethiopia


Ethiopia ni moja nya nchi maskini zaidi Afrika
Ethiopia imeweza kupunguza maradufu idadi ya vifo vya watoto wachanga wanaofariki wakiwa chini ya umri wa miaka mitano katika miongo miwili iliyopita , kulingana na takwimu za Umoja wa Maitaifa.
Ripoti ya UN inasema kuwa nchi hiyo imepunguza idadi ya vifo vya watoto hao hadi 68 kwa kila watoto elfu moja wanaozaliwa kutoka watoto 200 mwaka 1980.
Serikali imesema kuwa jambo hili zuri limetoakana na kukuwa kwa uchumi wake.
Hata hivyo licha ya idadi ya vifo vya watoto kupungua, shirika la watoto la UNICEF limesema kuwa Ethiopia inahitaji kujitahidi zaidi kuboresha taasisi zake za kiafya ili kuwahudumia vyema wanawake wajawazito.
Ethiopia ni moja ya nchi maskini zaidi Afrika ingawa imeshuhudia ukuwaji mkubwa wa uchumi wake katika miaka ya hivi karibuni. Pia ni moja ya nchi zenye kuzalisha kahawa kwa wingi Afrika.
Uchumi wa Ethiopia, unategeme kilimo ambacho kinahitaji mvua nyingi.
Mwandishi wa BBC mjini Addis Ababa, Emmanuel Igunza anasema Ethiopia ilikuwa moja ya nchi zilizokumbwa sana na janga la njaa.
Lakini kulingana na takwimu hizi za UN inadhihirisha kuwa Ethiopia ni moja ya nchi ambazo huenda zikaafikia lengo la Milenia la kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga.
Waziri wa Afya nchini humo Kesetebirhan Admasu anasema kuwa ongezeko la viwango vya ajira ndio sababu kubwa ya kuimarika kwa afya ya umma.

No comments:

Post a Comment