Baadhi ya wachezaji wa timu za Umisseta na Umitashumta, wakiwa katika hafla ya kuwapongeza iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam juzi. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wachezaji wa timu za Umisseta na Umitashumta, mkoni Dar es Salaam,wakiimba wimbo wa Taifa pamoja na wa Umisseta, wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert jijini.
Wachezaji wa timu za Umisseta na Umitashumta, mkoni Dar es Salaam, wakiimba wimbo nyimbo za Taifa na Umisseta, wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert jijini.
Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mratibu wa Umisseta, Kanda ya Dar es Salaam Brighton Mbasha akizungumza kwa ajili ya kutoa taarifa mbele ya mgeni rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana (wa pili kushoto), wakati wa hafla hiyo juzi.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando akizungumza katika hafla hiyo. Katikati ni Mgeni rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana na kulia ni Ofisa Elimu Mkoa, Raymond Mapunda.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando. akipokea kombe kutoka kwa Mussa Mikidadi, Kapteni wa mpira wa miguu.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando. akipokea kombe kutoka kwa Maria Rashid-kutoka Vijibweni.
Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana, akifurahia moja ya vikombe vilivyonyakuliwa na vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mashindano hayo yaliyofanyika Kibaha, mkoani Pwani.
Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana, akipena mikono ili kuwapongeza baadhi ya vijana baada ya kumkabidhi vikombe hivyo katika hafla hiyo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana akipokea moja ya vikombe vilivyo nyakulia na vijana wa Umisseta na Umitashumta mkoani Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana akikinyanyua juu moja ya vikombe vilivyonyakulia na vijana wa Umisseta na Umitashumta mkoani Dar es Salaam, wakati wa hafla hiyo ya kuwapongeza juzi.
Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana, akifurahia moja ya vikombe vilivyonyakuliwa na vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mashindano hayo yaliyofanyika Kibaha, mkoani Pwani.
Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana, akikifurahia moja ya vikombe vilivyonyakuliwa na vijana (kushoto) wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mashindano hayo, yaliyofanyika Kibaha, mkoani Pwani.
Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana, akikionesha moja ya vikombe hivyo, vilivyonyakuliwa na vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mashindano hayo yaliyofanyika Kibaha, mkoani Pwani, mara baada ya kukabidhiwa na vijana hao (kushoto), wakati wa hafla hiyo juzi.
Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana, akikionesha kwa wageni mbalimbali waliofika katika hafla hiyo moja ya vikombe hivyo,vilivyonyakuliwa na vijana wake wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mashindano hayo.
Hapa Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana, akiendela kuvionesha vikombe hivyo, vilivyonyakuliwa na vijana wa mkoani mwake, wakati wa hafla hiyo juzi.
Hapa kazi ikiendela vile vile, Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana, anakionesha moja ya vikombe hivyo, vilivyonyakuliwa na vijana wake wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando, akimkabidhi moja ya vikombe hivyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana, wakati wa hafla hiyo ya kuwapongeza vijana hao, ambao pia walinyakua ushindi wa jumla katika mashindano hayo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana, akiendelea kupokea na kuvionesha vikombe hivyo, wakati wa hafla hiyo juzi.
Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana, akimpongeza mmoja wa makapetini wa michezo mbalimbali ya mashindano hayo, wakati walipokuwa wakimkabidhi vikombe walivyojishindia na timu zao katika mashindano hayo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana akilinyanyua juu Kombe la Ubingwa wa jumla wa mashindano hayo, lililonyakuliwa na vijana wake wa Umisseta na Umitashumta wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa hafla hiyo ya kuwapongeza juzi.
Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana, Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando na Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda (kulia), wakilinyanyua juu kombe hilo la Ubingwa wa jumla mara baada ya kukabidhiwa na vijana wao hao, walioshiriki katika mashindano ya Umisseta na Umitashumta, Kibaha, mkoani Pwani.
Kaimu Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana akizungumza na wanamichezo hao pamoja na wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla hiyo ya kuwapongeza baada ya kuwa mabingwa wa michuano hiyo ya Umisseta na Umitashumta, iliyofanyia mkoani Pwani na kushirikisha nchi za Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment