TANGAZO


Friday, September 20, 2013

Uchaguzi wa wabunge Swaziland



Mfalme wa Swaziland Mswati wa tatu
Wapiga kura nchini Swaziland wanawachagua wabunge wapya. Nchi hiyo ina ufalme mdogo uliosalia Kusini mwa Afrika unaoongozwa na mfalme Mswati wa tatu.
Vyama vya kisiasa havijaharamishwa nchini humo, lakini vimedhibitiwa na ufalme huo. Wagombea wa nafasi za wabunge wa bunge lenye wanachama wa 55, wanachaguliwa na viongozi wa kitamaduni wanaomuunga mkono mfalme.
Wakosoaji wamepuuzilia mbali uchaguzi huo na kusema ni njia moja ya kuendelea kuidhinisha utawala wa mfalme. Hii ni licha ya baadhi ya watu wanaounga mkono mageuzi pia kuchaguliwa kwenye bunge hilo.
Changamoto kuu kwa ufalme itakuwa kukabiliana na viwango vya umaskini pamoja na upungufu pesa za matumizi ya serikali.

No comments:

Post a Comment