Timu ya Netiboli ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma kabla ya kukaguliwa kwa ajili ya mechi kati yake na timu ya netiboli ya Wizara ya Ujenzi katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma leo.
Timu ya Netiboli ya Wizara ya Ujenzi kabla ya kukaguliwa kwa ajili ya mechi kati yake na timu ya netiboli ya Utumishi katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma leo.
Timu ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma ikisalimiana na timu ya Wizara ya Ujenzi kabla ya mechi leo.
Mchezaji wa Timu ya Netiboli ya Utumishi Fatma Ahmed (GS) akidaka mpira hewani wakati wa mechi kati ya Utumishi na Wizara ya Ujenzi mjini Dodoma leo.
Mchezaji wa timu ya Ujenzi Bertha Wilson (GD) akitoa pasi wakati wa mechi kati ya Utumishi na Wizara ya Ujenzi mjini Dodoma.
Mchezaji wa Timu ya Netiboli ya Utumishi Fatma Ahmed (GS) akidaka mpira hewani wakati wa mechi kati ya Utumishi na Wizara ya Ujenzi mjini Dodoma leo.
Mchezaji wa timu ya Netiboli ya Utumishi Anna Msulwa (GA)(kulia) akifunga bao wakati wa mechi kati ya Utumishi na Wizara ya Ujenzi mjini Dodoma.
Mchezaji wa timu ya Netiboli ya Wizara ya Ujenzi Anjela Mvungi (GK) akidaka mpira wakati wa mechi kati ya Utumishi na Wizara ya Ujenzi mjini Dodoma.
Na
Happiness Shayo – Utumishi
Timu ya Netiboli ya Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeendelea kufanya vizuri katika mashindano
ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), kwa kuifunga
timu ya netiboli ya Wizara ya Ujenzi mabao 48-5 katika mchezo uliofanyika
kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma leo mchana.
Katika mechi hiyo,timu ya Utumishi
ilionekana kuumiliki mchezo kwa kiasi kikubwa kitendo kilichopelekea wachezaji
wa timu ya Wizara ya Ujenzi kutokujiamini na hatimaye kupoteza mabao yao kwa
wingi katika dakika ishirini za mwanzo ambapo Utumishi ilifunga mabao 12
kupitia mchezaji wake Fatma Ahmed (GS) na mengine 11 kupitia mchezaji wake Anna
Msulwa (GA).
Timu ya Wizara ya Ujenzi ilitumia
mbinu mbalimbali kurudisha mabao lakini ilifanikiwa kufunga bao 1 kupitia
mchezaji wake Kaundime Kizaba (GA).
Kipindi cha pili cha mchezo huo Utumishi
iliendelea kwa kasi ileile na kufanikiwa kuifunga timu ya Wizara ya Ujenzi
mabao 25 huku Ujenzi ikifunga mabao 4.
Akiongea mara baada ya mchezo huo
Kocha wa timu ya Wizara ya Ujenzi Bw.Abilai Ally alisema kuwa timu yake
imejitahidi sana katika kiwango chake kwa kuwa ni timu changa.
“Mchezo ni mzuri lakini timu yetu
bado ni changa kimashindano na ni mara ya kwanza kushiriki mashindano haya”
alisema Bw. Ally.
Aidha,alifafanua kuwa timu hiyo ina
upungufu wa wachezaji kitendo kilichopelekea kuelemewa na mchezo na kufungwa
mabao mengi.
Naye mchezaji wa timu ya Utumishi
Bi. Amina Ahmed (GD) alisema kuwa mchezo umeonekana mzuri kwa upande wa timu ya
Utumishi kwa sababu kila mchezaji ametumia nafasi yake vizuri kwa kucheza
inavyotakiwa.
Timu ya Utumishi yenye lengo la
kunyakua ubingwa katika mechi zijazo imeendelea kujinoa zaidi ili kufikia lengo
huku ikihakikisha haipotezi mchezo wowote katika michezo ya SHIMIWI
inayoendelea mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment