Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kufungua ofisi ya CCM Tawi la Nyabichune, Wilaya ya Tarime mkoani Mara.
Ofisi ya CCM Tawi la Nyabichune wilaya ya Tarime mkoani Mara ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilizindua rasmi leo tarehe 23 Septemba 2013.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nyamongo na kuwaeleza namna ambavyo wamejipanga kutatua tatizo la muda mrefu baina ya wakazi wa eneo hilo na wamiliki wa mgodi wa North Mara.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Nyamongo Chacha Magayo Butora ambaye alifafanua kwa kina matatizo yanayowakabili wakazi wa eneo hilo,Katibu Mkuu alitumia Demokrasia ya hali ya juu baada ya kuwapa nafasi watu watatu mbali mbali ambao wananchi waliwachagua waje kuelezea matatizo yao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyamongo wilaya ya Tarime mkoani mara ambapo aliamua kufuta kila kitu kwenye ratiba yake na kutaka wananchi wateue wawakilishi wao ili wakakae kikao na watu wa serikali ili kupata ufumbuzi wa matatizo hayo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele akifafanua mambo kadhaa ambayo Wizara yake inataka wananchi wafaidike na migodi ikiwa pamoja na kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo ambao wanatakiwa wajiunge kutengeneza vikundi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakiongea na wananchi wa Nyamongo ,Wananchi wa Nyamongo wameshukuru sana kwa kusikilizwa kwa ukaribu haijawahi tokea na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Viongozi hao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma moja ya taarifa inayofafanua matatizo ya wakazi wa Nyamongo.
Sehemu ya wakazi wa Nyamongo wakiwa kwenye kikao cha ndani pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Naibu Waziri Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele na Viongozi wengine wa Serikali ambapo walikaa na kujadili matatizo yao namna ya kuyatatua.
Na Mwandishi wetu
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana, leo amefanya ziara katika Wilaya ya Tarime Mkoani Mara .
Katibu Mkuu akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilazimika kupangua ratiba ya ziara ya baada ya kuona kuna jambo la muhimu zaidi angependa kupata muda na wakazi wa Nyamongo ambao wamekuwa na kero za muda mrefu bila kupata majibu.
Baada ya mapokezi katika kijiji cha Mrito, Katibu Mkuu alipokea taarifa ya kamati ya siasa kisha kuelekea katika shughuli ya kufungua Tawi la Nyabichune,mara tu shughuli za ufunguaji Tawi ilipokamilika alipokea taarifa mbali mbali na ndipo akagundua kuna haja ya kupangua ratiba na kwenda kusikiliza ya wananchi.
No comments:
Post a Comment