TANGAZO


Wednesday, September 18, 2013

Simba yashushia kipigo cha mbwa mwizi Mgambo JKT, yaipiga mabao 6-0

Mashabiki wa timu ya Simba, wakifuatilia timu yao wakati ilipopambana na Mgambo JKT ya Tanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Simba imeshinda mabao 6-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mashabiki wa timu ya Simba, wakifuatilia mchezo huo kati ya timu yao na Mgambo JKT ya Tanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. 
Amri Kiemba wa Simba (wa pili kushoto), akiwania mpira na Salum Mlima wa Mgambo JKT huku Mohamed Neto (kulia) wa timu hiyo, akisogea kwenda kutoa msaada. 
Amri Kiemba wa Simba (kushoto), akiwania mpira na Salum Mlima (katikati) na Mohamed Neto (kulia) wa Mgambo JKT wakati wa mchezo huo.
Mohamed Neto wa Mgambo JKT, akimtoka Gilbert Kaze wa Simba.
Gilbert Kaze wa Simba, akiutoa mpira miguuni mwa Mohamed Neto wa Mgambo JKT katika mchezo huo.
Amri Kiemba wa Simba wakiwania mpira na Mohamed Neto wa Mgambo JKT
Golikipa wa Simba, Abel Dhaira akipangua mpira wa juu uliokuwa ukiwaniwa kupigwa kichwa na Mohamed Nato wa Mgambo JKT
 Gilbert Kaze wa Simba, akiufuata mpira uliokuwa unadhibitiwa na Salum Mlima wa Mgambo JKT.
William Lucian wa Simba (kushoto) na Mohamed Nato wa Mgambo JKT, wakikimbilia mpira wa juu, wakati wa mchezo huo.
William Lucian wa Simba (kushoto) na Mohamed Nato wa Mgambo JKT, wakikimbilia mpira wa juu, wakati wa mchezo huo.

William Lucian wa Simba akiondoa mpira huo mbele ya Mohamed Nato wa Mgambo JKT.

William Lucian wa Simba, akipambana na Salum Gila wa Mgambo JKT.
 Hali ya mchezo ilikuwa mbaya kwa Mgambo JKT kwani hadi kipindi cha kwanza kinamalizika walikuwa tayari wameshalala kwa mabao 4-0 na mara tu baada ya kuanza kipindi cha pili Simba wakaiongeza bao la 5 kama inavyoonekana kwenye ubao wa matangazo uwanjani hapo.
 Amri Kiemba, akimtoka Salum Gila wa Mgambo JKT.
Gilbert Kaze wa Simba akiondoa mpira wa hatari uliokuwa ukielekezwa langoni mwa timu yake na Salum Gila, anaye pambana naye. 
Mashabiki wa Simba wakishangilia moja ya mabao ya timu hiyo yaliyofungwa katika mchezo huo.

Furaha ya ushindi, mashabiki wa Simba wakishangilia ushindi wa mabao 6 yaliyofungwa na timu yao katika mchezo huo.

Shabiki wa Simba akiwa na mdoli ulioshikilia kidoli kidogo kilichokuwa na rangi za timu mahasimu wao (Yanga), ikiwa ni kuonesha utani kwa wapinzani wao hao, waliotoka sare na Prison ya Mbeya kwa kufungana bao 1-1.

No comments:

Post a Comment