Rais Dk. Jakaya Kikwete, akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi mpya Dk. Luigi Scotto (kulia) kutoka Italia katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu- Dar es Salaam leo.
Rais Dk. Jakaya Kikwete, akizungumza na Balozi mpya anayeiwakilisha nchi ya Italia nchini Tanzania, Balozi Dk. Luigi Scotto (kushoto), leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi mpya anayeiwakilisha nchi ya Italia nchini Tanzania, Dk. Luigi Scotto (katikati waliovaa suti), akiwa pamoja na Maofisa Wakuu wa Itifaki, wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa leo kwenye hafla hiyo jijini.
Rais Dk. Jakaya Kikwete, akisikiliza taarifa ya utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Italia nchini Tanzania, Dk. Luigi Scotto (kulia), leo Ikulu Dar es Salaam.
Balozi mpya wa Italia nchini Tanzania, Dk. Luigi Scotto akisaini kitabu cha wageni leo, Ikulu jijini Dar es Salaam, alipokwenda kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Dk. Jakaya Kikwete.
Bolozi mpya wa Italia nchini Tanzania, Dk. Luigi Scotto (kulia), akisalimiana na baadhi ya Maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla hiyo. (Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.)
NA Eleuteri Mangi –Maelezo
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amepokea hati za utambulisho za Balozi mpya wa Italia katika Tanzania Dk. Luigi Scotto.
Mapokezi hayo yalifanyika katika halfa fupi iliyofanyika Ikulu leo jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete amemtaka Balozi huyo mpya kuisaidia kuyashawishi makampuni zaidi ya Italia kuja kuwekeza na kuboresha mahusiano ya kiuchumi wa baina ya nchi hizo mbili.
“Tumekuwa na makampuni makubwa ya Italia yaliyopata kuwekeza katika uchumi wa Tanzania ikiwa ni pamoja na Agip na Incar lakini bado tunahitaji uwekezaji zaidi ili tuweze kuimarisha zaidi uchumi wetu,” Rais Kikwete alimwambia Dkt. Scotto.
Aidha, Rais Kikwete ameishukuru Italia kwa misaada ambayo nchi hiyo imekuwa inatoa kuchangia maendeleo ya Tanzania ikiwamo kugharimia ujenzi wa Barabara ya Dar es Salaam Bagamoyo.
Naye Balozi huyo mpya kwa upande wake amesema kuwa amefurahi kuteuliwa kuwa Balozi katika Tanzania.
“Ndoto yangu kubwa tokea nikiwa mtoto ilikuwa ni kufanya kazi katika nchi iliyomtoa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere” alisema Balozi Scotto.
Balozi huyo alipowasili katika viwaja vya Ikulu alipokewa na wenyeji wake na nyimbo za mataifa hayo ziliimbwa zikiongozwa na bendi maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya mapokezi ya balozi.
Balozi Dkt. Scotto anachukua nafasi ya mtangulizi wake nchini Perluigi Velardi aliyemaliza muda wake wa kulitumikia taifa lake nchini.
No comments:
Post a Comment