TANGAZO


Thursday, September 12, 2013

Katibu Mkuu wa CCM Kinana azindua mradi mkubwa wa maji Mwigumbi, wilayani Kishapu

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mwigambi, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kutokana na Ilani ya CC, wilayni Kishapu, Shinyanga leo.
Wananchi wakishangilia viongozi wa juu wa CCM katika mkutano huo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama  Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mwigambi, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kutokana na Ilani ya CC, wilayni Kishapu, Shinyanga leo.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, akinawa uso kwa kutumia maji ya bomba baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Kinana kuzindua kisima kikubwa cha maji katika Kijiji cha Mwigambi, wilayani Kishapu leo.(PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Nape Nnauye akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama baada ya kisima cha maji kilichojengwa kwa thamani ya sh. mil 314 kuzinduliwa katika Kijiji cha Mwigumbi, wilayani Kishapu leo.(PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO)
 Nape Nnauye na Kinana wakinawa  baada ya kisima hicho kuzinduliwa rasmi  leo
 Kinana akizmtwisha ndoo ya majai mmoja wa akina mama wa kijiji hicho.
 Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Suleiman Nchambi akishiriki kucheza ngoma ya nyoka iliyokuwa ikitumbizwa na kikundu cha ngoma cha Makoyangi kutoka Isulilo, wilayani Maswa.
 Msanii Mashana Muhoboko wa kikundu cha ngoma cha Makoyangi, akiwa amebanwa na nyoka aliyekuwa akicheza naye wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisaidia kupaka rangi moja ya vyumba vya madarasa vinavyojengwa katika Shule ya Sekondari ya Mwigumbi, wilayani Kishapu leo. Kinana alichangia mifuko 20 ya simenti na mipita 10 ya soka na netiboli.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) na Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Suleiman Nchambi wakisaidia kuchekecha mchanga wa kujengea vyumba vya madarasa katika Shule ya Mwigumbi. 
Nape akichekecha mchanga. (Picha zote na Kamanda wa Matukio blog)

No comments:

Post a Comment