TANGAZO


Wednesday, August 28, 2013

Yanga, Costal Union nguvu sawa, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, zatoka bao 1-1.

Wachezaji wakiingia uwanjani kwa ajili ya kukaguliwa na kuanza mpira katika mpambano wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana blogspot.com)
Wachezaji wakiingia uwanjani kwa ajili ya kukaguliwa na kuanza mpira katika mpambano wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Wachezaji wakiingia uwanjani kwa ajili ya kukaguliwa na kuanza mpira katika mpambano wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Uhuru Seleman wa Costal Union (kulia) na Juma Abdul wa Yanga, wakikimbilia mpira wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Uhuru Seleman wa Costal Union akimtoka Juma Abdul wa Yanga, hukua akizengewa na Nadir Haroub 'Canavaro' wa timu hiyo wakati wa mchezo huo jijini Dar es Salaam leo, Uwanja wa Taifa.
Uhuru Seleman wa Costal Union, akijaribu kumpiga chenga Juma Abdul wa Yanga, wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Haruna Moshi 'Boban' wa Costal Union akijaribu kumpiga kanzu Nadir Haroub (23) wa Yanga katika mchezo huo, Uwanja wa Taifa leo.
 Mashabiki wa timu ya Costal Union,wakifuatilia mchezo huo, uwanjani hapo.
 Mashabiki wa timu ya Yanga, wakifuatilia mchezo huo, uwanjani hapo. Timu hizo zilifungana bao 1-1.
 Didier Kavumbagu wa Yanga, akijaribu kumhadaa Marcus Ndehele wa Costal Union.
Didier Kavumbagu wa Yanga, akijaribu kuutoa mpira miguuni mwa Marcus Ndehele wa Costal Union.
Haya ni matokeo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika katika mchezo huo.
 Abdi Banda wa Costal Union akimdhibiti mshambuliaji Simon Msuva wa Yanga katika mchezo huo.
Golikipa Shaabaan Kado wa Costal Union akijiweka tayari kuudaka mpira wa kichwa uliokuwa ukipigwa na Simo Msuva wa Yanga.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao leo lililofungwa na Didier Kavumbagu (katikati) katika mchezo huo.
Hadi wakati huo, ubao wa matangazo ulikuwa ukionesha Yanga bao 1, Costal Union 0.


Nadir Haroub 'Canavaro' wa Yanga, akipiga shuti mbele ya Marcus Ndehele wa Costal Union wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, ulichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, baada ya Jerry Santo kuisawazishia Costal Union kwa njia ya penalti.

No comments:

Post a Comment