Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uchunguzi na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wizara yake, ikiwemo kuwafukuza kazi na baadhi yao kuwavua vyeo Askari Polisi waliokiuka maadili ya kazi zao. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uchunguzi na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wizara yake, ikiwemo kuwafukuza kazi na baadhi yao kuwavua vyeo Askari Polisi waliokiuka maadili ya kazi zao. Kushoto ni Naibu wake, Pereira Ame Silima.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uchunguzi na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wizara yake, ikiwemo kuwafukuza kazi na baadhi yao kuwavua vyeo Askari Polisi waliokiuka maadili ya kazi zao. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbaraka Abdulwakili.
Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari, wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo, kuhusu uchunguzi na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wizara yake, ikiwemo kuwafukuza kazi na baadhi yao kuwavua vyeo Askari Polisi waliokiuka maadili ya kazi zao.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uchunguzi na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wizara yake, ikiwemo kuwafukuza kazi na baadhi yao kuwavua vyeo Askari Polisi waliokiuka maadili ya kazi zao. Kushoto ni Naibu wake, Pereira Ame Silima.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uchunguzi na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wizara yake, ikiwemo kuwafukuza kazi na baadhi yao kuwavua vyeo Askari Polisi waliokiuka maadili ya kazi zao. Kushoto ni Naibu wake, Pereira Ame Silima.
UCHUNGUZI
WA MATUKIO YALIYOLALAMIKIWA DHIDI YA ASKARI POLISI KATIKA MIKOA YA ARUSHA,
KILIMANJARO, MOROGORO NA KIGOMA
Kati
ya tarehe 26 Desemba 2012 na tarehe 18 Mei 2013, yametokea matukio mbalimbali
katika Jeshi la Polisi yaliyolalamikiwa na wananchi na kuandikwa kwenye vyombo
vya habari. Baadhi ya matukio hayo ni yafuatayo:-
1.
Tukio
la gari la Kikosi cha Kutuliza Ghasia kutumika katika uhalifu (ubebaji wa
bangi) katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
2.
Polisi
Mkoa wa Morogoro kutumia fuvu la kichwa cha binadamu kumbambikizia
mfanyabiashara kwa lengo la kupata fedha.
3.
Mauaji
ya mfanyabiashara wa Wilaya ya Kasulu yaliyofanywa na Askari wawili wa Jeshi la
Polisi.
Baada ya kuyapokea malalamiko hayo,
niliunda Kamati ya kuyachunguza ili kubaini ukweli. Kamati imefanya kazi
niliyowatuma na kunikabidhi Taarifa ya Uchunguzi. Baada ya kuipitia Taarifa
hiyo kwa makini nimeridhia maoni ya Kamati na hivyo tumefanya maamuzi
yafuatayo:
1.0
TUKIO
LA BANGI
Tukio hili lilitokea tarehe 18 Mei 2013 majira ya saa tano na nusu za
usiku maeneo ya Kilema Pofu katika barabara ya Himo Moshi Mkoani
Kilimanjaro. Kufuastia tukio hilo,
waliokuwa Askari Polisi Ex F.1734 Cpl Edward wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia
Mkoa wa Arusha na Ex G.2434 PC George
wa Kituo cha Polisi Ngarananyuki, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha walifukuzwa
kazi tarehe 20/05/2013 baada ya kukiri kosa la kusafirisha bangi kwa kutumia
gari ya Polisi.
1.1
Katika
tukio la gari lenye usajili PT 2025 Toyota Land Cruiser la Kikosi cha Kutuliza
Ghasia Mkoa wa Arusha kutumika katika ubebaji wa bangi yenye uzito wa kilogramu
540 zenye thamani ya Tshs 81,000,000/= kukamatwa mkoani Kilimanjaro usiku wa
tarehe 18 Mei, 2013, Mkuu wa Kikosi hicho Mkarakibu wa Polisi Ramadhan Giro amevuliwa madaraka aliyonayo kwa kushindwa
kuwasimamia kikamilifu Askari na Maafisa walio chini yake na kusababisha hilo
kutokea.
1.2
Kitendo
cha Inspekta Isaack Manoni kutuhumiwa kumtorosha mtuhumiwa hatari Ex F.1734 Cpl
Edward aliyekuwa
dereva wa gari la Jeshi la Polisi lililokamatwa na bangi Mkoani Kilimanjaro ni
cha kulifedhehesha Jeshi la Polisi. Hivyo, Inspekta Isaack Manoni amesimamishwa kazi na nimeagiza
ashtakiwe kijeshi.
1.3
Kitendo
cha Inspekta Salum Juma Kingu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Kilimanjaro kubaki
kwenye gari umbali wa mita 80 kutoka nyumba ya mtuhumiwa Ex F.1734 Cpl
Edward wakati Cpl
Edward alipokuwa
amepelekwa kutoka Moshi kukabidhi vifaa vya Jeshi la Polisi, kilichangia
mtuhumiwa kutoroka. Inspekta Salum Juma Kingu amepewa onyo na anatakiwa kuwa
makini katika utendaji kazi wake.
1.4
Inspekta
Mikidadi Galilima
hakutimiza wajibu wake ipasavyo katika kumshauri Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia
Mkoa wa Arusha katika ukaguzi na usimamizi wa rasilimali za kikosi. Aidha,
kitendo chake cha kujaribu kuficha ukweli kwa kuelekeza matairi mapya
yaliyonunuliwa na Ex F.1734 Cpl Edward yavuliwe na yarejeshwe ya zamani kwenye gari PT. 2025
baada ya uhalifu ni cha kukosa uadilifu kama kiongozi. Inspekta Mikidadi
Galilima amepewa onyo
kali.
1.5
PF
15828 ASP Francis S. Duma aliyekuwa kiongozi katika tukio la kukamata gari ya Jeshi la Polisi
lililokuwa limebeba bangi Mkoani Kilimanjaro amepandishwa cheo kuwa Mrakibu
wa Polisi kuanzia
jana tarehe 21/08/2013. Aidha,
Askari 14 aliokuwa nao siku hiyo ya tukio wapongezwe kwa kupewa zawadi inayostahili ndani ya mamlaka ya IGP.
2.0 TUKIO LA FUVU
Tarehe 07 Mei, 2013
Askari watatu wa Jeshi la Polisi Ex E.4344 D/Sgt Mohamed
na Ex E.3861 Cpl Nuran wa kituo cha Polisi Dumila na
Askari Polisi Ex D.4807 D/SSgt Sadick Madodo wa kituo
cha Polisi Dakawa wakishirikiana na raia wawili matapeli Rashid Hamis @ Shariff
na Adam Peter @ Saloon walimbambikizia fuvu la kichwa cha
binadamu mfanyabiashara Bw. Samson Mwita @Kihindi
wa Dumila, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kupata fedha. Askari
hao wamefukuzwa kazi na wameshtakiwa kwa uhalifu waliotenda.
Kabla ya tukio hili Inspekta Jamal Ramadhan
ambaye ni Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Mvomero alikuwa na taarifa ya mpango wa
kufanyika utapeli katika maeneo ya Dakawa na Dumila ambapo matapeli walikuwa wanapanga kwa kushirikiana na Askari Polisi wasio waaminifu kuwabambikizia
watu kesi kwa lengo la kupata fedha, lakini hakumtaarifu Mkuu wa Kituo cha
Polisi Dumila. Aidha, Mkuu wa
Kituo cha Polisi Dumila Inspekta Juma Mpamba ameonesha
udhaifu katika utendaji kazi wake kwa kutosimamia kikamilifu Askari walio chini
yake, kitendo kilichosababisha Askari hao kujipangia kazi nje ya utaratibu,
hivyo kuwa na ujasiri wa
kumbambikizia mfanyabiashara kesi kwa kutumia fuvu la kichwa cha binadamu kwa
lengo la kujinufaisha kinyume na maadili ya kazi.
Aidha, Inspekta huyu alishindwa kumfuatilia na kumkamata tapeli maarufu Bw.
Adam Peter @ Saloon aliyekuwa kinara wa tukio hili hadi Kamati ilipotoa
msisitizo na shinikizo la kukamatwa
kwa tapeli huyo. Kutokana na kasoro zilizoainishwa dhidi ya Inspekta
Jamal Ramadhan na Inspketa Juma Mpamba,
wote wamevuliwa madaraka walionayo.
3.0 TUKIO LA KASULU
Tarehe
25 Disemba, 2012 usiku wa kuamkia tarehe 26 Disemba, 2012 katika Kituo Kidogo
cha Polisi Heru UShingo kilichopo Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, Askari
Polisi Ex D.8622 Cpl Peter na Ex G.1236 PC Sunday
kwa pamoja walimpiga marehemu Gasper Mussa @ Sigwavumba
mwenye umri wa miaka 36 na kisha kumweka katika Mahabusu ya Kituo hicho bila
msaada wowote wa matibabu hatimaye kufariki tarehe 26 Disemba, 2012 majira ya
asubuhi kutokana na kupasuka kwa bandama. Upelelezi mbovu uliofanywa chini ya
usimamizi wa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kasulu ASP Daniel Bendarugaho
katika kesi ya mauaji dhidi ya Askari hao ambao tayari walikuwa wameshafukuzwa
kazi ulisababisha kesi kuondolewa Mahakamani.
Kutokana
na kitendo cha Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kasulu ASP Daniel Bendarugaho
kutokuwa makini katika kufanya na kusimamia upelelezi wa jalada husika la kesi
ya mauaji ya marehemu Gasper Mussa Sigwavumba; ASP
Daniel Bendarugaho amevuliwa madaraka aliyonayo. Aidha, upelelezi wa kesi hiyo utaanza
upya ili haki itendeke.
Dkt Emmanuel J. Nchimbi (MB)
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
22/08/2013.
No comments:
Post a Comment