TANGAZO


Tuesday, August 20, 2013

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI (GPSA), Yaelezea mchango wake katika kupunguza gharama za ununuzi Serikalini

Mkurugenzi Himili Biashara wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini, Malick Sanga (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, juu ya mfumo mpya wa kadi maalum (Smart Card), utakao tumiwa na madereva wa Serikali kupata wa huduma ya ununuzi wa mafuta ya gari na kulia ni Mkurugenzi wa Ununuzi na Ushauri wa Wakala hao, Yoswam Nyongera.
Mkurugenzi wa Ununuzi na Ushauri wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Yoswam Nyongera akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchago wa wakala hao katika kupunguza gharama za ununuzi serikalini wakati wa mkutano na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa. (Picha zote na Frank Mvungi, Maelezo)

1.      UTANGULIZI
Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) ulianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali sura ya 245 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 na kutangazwa katika Gazeti la Serikali Na.235 la tarehe 7 Desemba, 2007. Wakala ulizinduliwa rasmi tarehe 16, Juni 2008. GPSA ina ofisi katika kila mkoa Tanzania bara na iko chini ya Wizara ya fedha.
        Kuanzishwa kwa GPSA ni matokeo ya Program za uboreshaji wa utendaji katika sekta ya umma (Public Service Reforms Program-PSRP) ambapo katika maboresho hayo iliyokuwa Bohari kuu ya Serikali ilifutwa na baadhi ya majukumu yake yalichukuliwa na GPSA.

2.      MAJUKUMU YA WAKALA

Majukumu ya Wakala kama yalivyoainishwa kwenye ‘Hati ya idhinisho Na. 235 ya tarehe 7 Desemba  2007 ikisomwa kwa pamoja na marekebisho yake kupitia Gazeti la Serikali Na. 133 la  tarehe13 Aprili 2012;  ni pamoja  na:
(i)           Kuuza vifaa  na mafuta ya magari kwa Taasisi za Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali,
(ii)        Kuandaa taratibu za ununuzi wa vifaa na huduma mtambuka kwa ajili ya wizara, Idara na Taasisi za Umma,
(iii)      Kuandaa na kutunza orodha ya wauzaji vifaa na watoa huduma mtambuka,
(iv)      Kugomboa mizigo ya Serikali na Taasisi zake kutoka  bandarini, viwanja vya ndege na mipakani na Kutoa ushauri katika maeneo ya ununuzi; ugavi na ugomboaji wa mizigo
(v)         Kupangisha maghala na maeneo ya wazi na
(vi)      Kukodisha magari ya mizigo.
3.            GHARAMA ZA UNUNUZI KATIKA SEKTA YA UMMA
·         Ununuzi katika Sekta ya Umma ni eneo ambalo linatumia fedha nyingi za Serikali
·         Inakadiriwa kuwa asilimia takribani 70-80 ya bajeti ya Matumizi ya kawaida ya Serikali hutumika katika ununuzi
·         Gharama za ununuzi zinahusika na i) uendeshaji mchakato wa zabuni na  ii) bei ya kununulia kifaa/huduma
·         Kutokana na matumizi makubwa ya fedha katika eneo hili Serikali inao mfumo wa ununuzi wa pamoja wa Vifaa na Huduma Mtambuka ambao unasimamiwa na GPSA na unalenga katika kupunguza gharama za ununuzi.Mfumo huu unaziwezesha taasisi za umma   kupata mahitaji yao haraka bila kuendesha mchakato wa zabuni.
·         Mfumo huu umegawanyika katika sehemu kuu mbili (sub-systems) ambazo ni:
3.1.1    Ununuzi, Utunzaji  na Usambazaji wa Vifaa kwa ajili ya kuuza katika    Taasisi za Umma
GPSA   inanunua na  kutunza na kusambaza  vifaa vinavyohitajika katika taasisi za umma. Bidhaa/vifaa vinavyopatikana moja kwa moja kutoka  ofisi za GPSA ni pamoja na bendera za taifa, Vifaa vya Ofisini, Shajala, Kalenda,Vifaa vya usafi, Mafuta ya magari na mitambo
Utaratibu wa kununua kwa pamoja vifaa vinavyohitajika katika taasisi za umma unapunguza gharama za kuendesha mchakato wa ununuzi unaofanywa na kila taasisi ya umma lakini pia utaratibu huu ni mkakati (strategy) wa Serikali wa kuwa na chombo chake kinachoweza kutumika wakati wowote kutoa huduma katika mazingira ya dharura kama vile mafuriko,vita,migomo ya wafanyabiashara kazi maalum za serikali n.k.Bidhaa zinazopatikana GPSA zinauzwa kwa Taasisi za umma tu.
3.1.2        Mfumo wa Ununuzi wa Pamoja wa Vifaa na Huduma Mtambuka ambazo    hazipatikani GPSA
GPSA inaandaa pia utaratibu wa ununuzi wa pamoja wa  Vifaa na Huduma Mtambuka(VHM) ambazo hazipatikani GPSA.         VHM ni vile ambavyo vinahitajika kila wakati au mahitaji yake yanajirudia katika taasisi za umma. VHM ambazo hazipatikani GPSA zimeandaliwa mfumo maalum ambao unaziwezesha taasisi za umma kupata mahitaji yao bila kulazimika kuendesha mchakato mzima wa zabuni na kwa kufuata sheria.
Pale ambapo vifaa na Huduma hazipatikani GPSA au pale ambapo   GPSA haiwezi kufikisha huduma zake katika maeneo yote ambako taasisi za umma zinapatikana, mfumo huu unasaidia kufikisha huduma kwenye maeneo yote zilipo taasisi za umma kupitia wazabuni walioteuliwa kuuza bidhaa na huduma Mtambuka.
 Kwa utaratibu huu  GPSA hutangaza zabuni za VHM na kuendesha mchakato wa zabuni hadi kutoa mikataba maalum kwa waombaji waliotimiza masharti ya zabuni.Mikataba maalum inayotolewa na GPSA hutumiwa na Taasisi nunuzi kuagiza VHM.


4              MAFANIKIO KATIKA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UNUNUZI KWA SERIKALI
GPSA katika kusimamia na kuendesha mfumo wa ununuzi wa pamoja imeweza kuuza vifaa na mafuta katika taasisi za umma,kuandaa mikataba maalum kwa VHM  ambazo hazipatikani GPSA,ambapo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita thamani ya vifaa na mafuta yaliyouzwa ni kama ifuatavyo:-
S/N
MWAKA
THAMANI YA VIFAA NA MAFUTA VILIVYOUZWA
1
2010/2011
25.9 bn
2
2011/2012
31.5 bn
3
2012/2013
31.2 bn
Aidha tangu kuanzishwa kwa mfumo wa ununuzi wa pamoja wa VHM mwaka 2009/2010, idadi ya Taasisi za umma  na thamani ya ununuzi  wa VHM kupitia mikataba maalum      (Framework agreements) ni  kama inavyoonekana hapa chini:-
NA
MWAKA
IDADI YA TAASISI ZILIZOTUMIA MIKATABA
THAMANI YA UNUNUZI
1
2009/2010
47
1.9bn
2
2010/2011
102
24.7bn
3
2011/2012
150
28.5bn
4
2012/2013
60
5.4 bn-(Bado taarifa  zinakusanywa)
5              MIKAKATI YA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA NA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UNUNUZI
·         Kuanzisha mfumo wa ki-electronik kuendesha mchakato wa  zabuni                (e-tendering)
·         Kuanzisha mfumo wa ki-electronik (smart card) kuuza mafuta kwa magari ya Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali
·         Kuagiza na kununua vifaa na mafuta kutoka kwa wazalishaji wa ndani na nje ya nchi ili kudhibiti ubora wa bidhaa hizo kwa  wakati wote na kwa bei ya ushindani.
·         Kuongeza wigo wa bidhaa zinazouzwa na GPSA (mfano, Consumables for Office equipment)
·         Ununuzi wa magari ya Serikali kwa pamoja
6              FAIDA ZA KUTUMIA MFUMO WA UNUNUZI WA PAMOJA
Faida zitokanazo na ununuzi wa pamoja ni pamoja na :-
·         Kupunguza gharama za mchakato wa zabuni
·         Kuondoa tofauti kubwa katika bei ya vifaa na huduma baina ya taasisi moja na nyingine;
·         Kutoa nafasi kwa taasisi nunuzi kujihusisha zaidi na majukumu ya msingi ya taasisi husika badala ya kutumia muda mwingi kwenye masuala ya ununuzi
·         Kupunguza muda wa kupata vifaa kwani mara tu vinapohitajika vinaagizwa bila kuanzisha mchakato wa zabuni
·         Kupunguza gharama na muda wa wafanyabiashara katika  kushiriki kwenye zabuni za umma
·         Kutoa fursa sawa kwa wafanyabiashara katika ushiriki wa zabuni pindi zinapotangazwa;
·         Zabuni hutangazwa na mikataba maalumu hutolewa kwa kufuata maeneo (mikoa), hivyo kutoa fursa zaidi  kwa wafanyabiashara kuomba maeneo watokayo kwa kuzingatia utaratibu uliopo;

Kiambatisho Na.1
MAENEO YANAYOHUSU GHARAMA ZA KUENDESHA MCHAKATO WA  ZABUNI
a)         Vikao vya Bodi ya zabuni kuidhinisha rasimu ya kitabu cha zabuni            
b)        Kuandaa vitabu vya zabuni  
c)         Matangazo
d)        Ufunguzi wa zabuni
e)         Tathmini ya zabuni
f)          Bodi ya zabuni kuidhinisha utoaji wa mkataba  
g)        Matangazo ya matokeo ya zabuni
Inakadiriwa kuwa gharama ya kuendesha mchakato wa zabuni moja ni takribani sh.millioni kumi hadi kumi na tano ,Kila taasisi ikiendesha mchakato wa zabuni ni lazima itaingia  gharama  zinazotokana na kazi zilizotajwa hapo juu.
            Gharama hizi zinapungua  mchakato wa zabuni unapoendeshwa na taasisi moja kwa niaba ya  taasisi zote.

 kiambatisho Na.2
ORODHA YA VIFAA VINAVYOPATIKANA GPSA
CLASS  TWO
S/N
ITEM
DESCRIPTION
UNIT
1
0555
Soft Brooms
Ea
2
0701
Keyrings
Ea
3
0702
Souvernirs
Ea
4
0703
Brass Lapel Pin - Gold
Ea
5
0704
Hand Flags
Ea
6
0705
National Flag Car - Normal
Ea
7
0706
National Flag Table - Normal
Ea
8
0707
Brass Lapel Pins
Ea
9
0708
Natioanl Flag Table
Ea
10
0709
Brass Lapel Pin - English
Ea
11
0709
Brass Lapel Pin - Swahili
Ea
12
0709 B
Brass Lapel Pin - Presidential
Ea
13
0710
National Flag Car
Ea
14
0711
National Flag Boat
Ea
15
0712
National Flag Pole
Ea
16
0715
Presidential Car Flag
Ea
17
0715
Presidential Car Flag
Ea
18
0716
Presidential Flag - Pole
Ea
19
0717
Natioanal Flag - Large
Ea
20
0721
Tarpulins Complete
Ea
CLASS  THREE
S/N
ITEM No.
DESCRIPTION
UNIT
1
4849
Roofing Nail
Ea
CLASS  FOUR
S/N
ITEM No.
DESCRIPTION
UNIT
1
189
Fluorescent Fitting
Ea
2
5003
Electric Cooker
Ea


CLASS  SIX
S/N
ITEM No.
DESCRIPTION
UNIT
1
6002
Office glue
Bot
2
6007
CRIN books
Ea
3
6008
Carbonized CRIN books
Ea
4
6016
Counter Book 2Quire
Ea
5
6017
Counter Book 4Quire
Ea
6
6018
Dispatch Book
Ea
7
6019
Note book spiral
Ea
8
6022
Writing Pad
Pad
9
6023
Sticker Paper
Pad
10
6026
Draft Pad
Pad
11
6035
Visitors Book
Ea
12
6036
Log Books
Ea
13
6060
Calender
Ea
14
6060
Calender
Ea
15
6064
Diaries
Ea
16
6064
Diaries 2013
Ea
17
6091
Paper Clips
Box
18
6133
Duplicating Ink
Tube
19
6152
Envelop Small size
Pkt
20
6153
Envelopes Q Size
Pkt
21
6153
Envelopes Small Size
Pkt
22
6158
Envelopes M/Size
Pkt
23
6160
Envelopes L/Size
Pkt
24
6192
File Cover  General
Pkt
25
6199
File Liver Arch
Ea
26
6203
Box File
Ea
27
6207
File Cover Confidential
Pkt
28
6281
Photocopy paper
Rm
29
6294
Carbon Paper Blue
Ea
30
6296
Duplicating Paper
Ream
31
6320
Minute sheet
Ea
32
6327
Typing Paper
Ream
33
6328
Carbon paper Red
Ea
34
6375
Ball Pen
Doz
35
6400
Office Pins
Ea
36
6410
Punching Machine 1 hole
Ea
37
6411
Punching Machine 2 holes
Ea
38
6415
Typewriter
Ea
39
6427
Ribbon for Typewriter
Ea
40
6447
Staple Pins
Pkt
41
6581
Green Tags
Ea
42
6648
Dustless Chalk Red
Ea
43
6649
Spiral Note Book A4
Ea
44
6650
Spiral Note Book 100pg
Ea
45
6651
Counter Book 1Quire
Ea
46
6652
Counter Book  Q3
Ea
47
6653
Constitution-Kiswahili
Ea
48
6654
Constitution -English
Ea
               CLASS 50
S/N
ITEM No.
DESCRIPTION
UNIT
1
0014
Diesel
Ltr
2
0022
Motor Petrol
Ltr

                                                                                                                            Kiambatisho Na.3
        ORODHA YA  MAKUNDI YA VIFAA NA HUDUMA MTAMBUKA
Na.
                                    KUNDI
1.
Stationery and Office Supplies
2.
Office Equipment & Consumables
3.
Furniture and Fittings
4.
Cleaning Materials and Supplies
5.
Motor vehicle Accessories
6.
Food and Beverages
7.
Uniform, Beddings, Sports Gears and Textile Materials
8.
Laboratory Supplies
9.
Kitchen Appliances
10.
Building Materials, Machinery and Hardware
11.
Fire wood
12.
Fuels and Lubricants
13.
Textbooks for schools and Teaching Colleges
14.
Catering services
15.
Conference and Related Services
16.
Cleaning services
17.
Fumigation services
18.
Security services
19.
Air Travel and Hotel Reservation services
20.
Transport and Handling Services
21.
Service and Maintenance of Office Equipment
22.
Service and Maintenance of Fire Fighting Equipment
23.
Grinding and Milling Services
24.
Service and Maintenance of Elevators
25.
Service and Maintenance of Fire Security System
26.
Hiring Photocopying Services Using Vendor management Inventory System
27.
Clearing and Forwarding Services
28.
Internet Services
29.
Documentary Services
30.
Courier Services
31.
Insurance Brokage Services


1 comment:

  1. Dear Customers,
    Expert funding group provides loans to Individuals and companies especially Individuals who have business plans and Ideas but find it difficult to start due to low or lack of starting capital.

    Business ideas with low investment and high profit you can start.
    Supermarket and fast food restaurant stores.
    Clothing and jewelry Sector etc.

    Get an Instant Short and long term loan to Set up your own business and enjoy the benefits of being your own boss.

    with an affordable 2% interest rate
    Flexible repayment 1 to 15 years duration
    Contact us via email: franchisecapitalcorps@gmail.com

    ReplyDelete