Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki moon amesema matumizi ya silaha za kikemilkali nchini Syria utakuwa ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.
Katika hotuba ya kuadhimisha karne ya Umoja wa Matifa ya mpango wa amani, Bwana Ban amesema ni muhimu wachunguzi wa Umoja wa Mataifa waliopo nchini Syria kuwa na muda wa kutosha kufanya kazi yao.
Bwana Ban amesema wamekusanya sampuli za maana na kuwahoji wahanga na walioshuhudia tukio hilo.
Alirejelea wito wake wa kuzitaka pande mbili zinazozozana nchini humo kusitisha mapigano na kuanzisha mazungumzo ya amani.
Katibu huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa anasema jamii ya kimataifa haiwezi kukaa kimya huku watu wa Syria wakiumia .
''Tumefikia kipindi kibaya katika mzozo huu'' Ban Ki-Moon aliuambia ukumbi uliojaa wanadiplomasia wa kigeni, kwamba matumizi ya aiana yoyote ya silaha za kemikali ni ukiukaji mkubwa wa sheria ya kimataifa na kuwa watakaohusika ni sharti wawajibishwe.
Katibu huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema ni lazima jamii ya kimataifa ifanye juhudi zote zinazowezekana kuzikutanisha pande husika katika meza ya mazungumzo.
Akikamilisha hotuba yake Bwana Ban alisema '' Mzozo wa Syria ni changamoto kubwa la vita na amani katika dunia ya sasa na kuwa watu wa Syria wanahitaji suluhu ya haraka na wala sio kimya.
Je Syria itashambuliwa Kijeshi?
Rais Barack Obama wa Marekani na waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron wameafikiana kuwa ni dhahiri silaha za kikemikali zilitumika katika mashambulio ya wiki jana nchini Syria na kwamba serikali ya rais Bashar Al Assad ndiyo iliyohusika.
Hata hivyo waziri mkuu David Cameron hajatoa ishara yoyote ikiwa watatumia nguvu za kijeshi kutatua mzozo huo Syria .
Lakini katika mahojiano na BBC na vyombo vingine vya habari alisisitiza kuwa hatua yoyote itakayochukuliwa italenga kujibu matumizi ya silaha za kemikali.
Licha ya kwamba chama cha upinzani cha Labour kimeonysha ishara kwamba kinaweza kuunga mkono uingiliaji kati wa jeshi nchini Syria wengi wa wanasiasa bado hawajaamua.
Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa anatarajiwa kuwasilisha azimio kuhusu Syria wakati wa mkutano wa Baraza la usalama wa Umoha wa Mataifa
Cameron amesema azimio hilo ni la kulaani serikali ya rais Bashar Al Assad kwa kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia wake na pia kuidhinisha mikakati maalum ya kulinza raia wa Syria.
Bwana Cameron amesema serikali yake inataka Umoja wa Mataifa kuwajiabika katika mzozo huo wa Syria.
Tangazo hilo limetolewa baada ya rais Obama kushauriana kwa njia ya simu na rais Barrack Obama wa Marekani.
Marekani bado haijatoa ripoti yake ya ujasusi kuhusu shambulio hilo, lakini vyombo vya habari nchini marekani vinadai kuwa uchunguzi huo ulidukua mawasiliano kati ya maafisa wa wizara ya ulinzi nchini Syria wakikubali kutekeleza shambulio hilo.
No comments:
Post a Comment