TANGAZO


Saturday, August 24, 2013

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete azindua Baraza la Ushauri la Wazee Mjini Dodoma


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, akiwasili kwenye viwanja vya Makao Makuu ya chama Dodoma, tayari kwa ufunguzi wa Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama. Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho Taifa, Abdulrahman Kinana na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Zanzibar, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Makamu Mwenyekiti CCM Bara, Mstaafu John Malecela, kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana, Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar, Aman Karume, wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama.
Wasanii wa Kundi la Kyela Beats wakitumbuiza wakati wa sherehe za kuzindua Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM, leo Agosti 24,2013.
Katibu wa CCM Taifa ,Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa salaam za utangulizi wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ushauri la Wazee la CCM.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wajumbe wa halmashauri kuu pamoja na wanachama wa CCM wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete akiwa pamoja na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wastaafu wa Chama wanaounda Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama.

No comments:

Post a Comment