TANGAZO


Tuesday, August 20, 2013

Msafara wa Mwenge wapata ajali Wilaya ya Dodoma Mjini



Msafara wa Mwenge ukiwa katika eneo uliopata ajali wakati ukikimbizwa Wilaya ya Dodoma Mjini leo. (Picha zote na John Banda)
 Majeruhi akipatiwa huduma ya kwanza

  Majeruhi akipatiwa huduma ya kwanza
 Moja ya gari ya msafara wa mwenge iliyopata ajali kwa kugongwa nyuma.
 Jiwe lililosababisha ajali hiyo (mbele ya tairi la gari kulia), likiwa limesimama.
 Baadhi ya magari yaliyogongana katika ajali hiyo.
 Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo, akipatiwa huduma ya kwanza kwenye mguu wake wa kulia.
 Majeruhi wa ajali hiyo, akifungwa bendeji mguuni.
 Majeruhi mwingine akipewa huduma ya kwanza.
Kituo cha kupokela mwenge huo, wilayani Mpwapwa, wananchi wakiusubiri mwenge huo.

Na John Banda, Dodoma
MBIO za Mwenge wa Uhuru, uliokuwa ukikimbizwa katika Wilaya ya Dodoma mjini, zimeingia dosari baada ya kupata ajali kilometa 3 kabla ya kukabidhiwa wiliya ya Mpwapwa.

Ajali hiyo iliyotokea leo majira ya 2:24 asubuhi katika mteremko wa Mlima Fufu wilayani Chamwino na kusababisha watu 5 kujeruhiwa na kukimbizwa katika Hospital ya Mkoa ya General.

Watu hao ambao majina yao bado hayajatambulika, walipata majeraha katika sehemu mbalimbali ya miili yao, ikiwemo kichwani, kifuani, miguuni na mikononi.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Suzan Kaganda aliyefika na kujione hali ilivyokuwa katika eneo hilo, alisema chanzo cha ajali hiyo ni matuta yaliwekwa kwenye Barabara hiyo, inayojengwa kwa kiwango cha lami toka Fufu hadi Dodoma bila kuwa na alama yoyote.

Kaganda alisema baada ya gari la polisi lililokuwa likiziongoza mbio hizo za mwenge pamoja na lililokuwa limeubeba kupita ndipo ajali hiyo ikatokea baada ya gari la nyuma kupanda moja ya mawe yaliyokuwa kwenye matuta na kufunga breki hafla.

“Kutokana na vumbi jingi lililokuwa kwenye barabara hiyo, kutokana na msafara wa magari mengine, gari la nyuma lililigonga kwa nyuma na mengine yakafuata kiasi cha kufikia jumla ya magali 7 huku 5 yakishindwa kuendelea na msafara huo’’, alisema Kaganda.

Aidha, aliongeza kuwa msafara huo uliendelea na kukabidhiwa wilaya ya Mpwapwa tukio likifanywa na Lepphy Gembe wa Dodoma mjini na Chrstopher Kangoye wa Mpwapwa.

Mbio hizo za mwenge Kitaifa ziliongozwa na Jama Ali Simai zenye ujumbe wa amani, Tusigawanywe kwa misingi ya tofauti zetu za Dini, itikadi, Rangi na Rasilimali.

No comments:

Post a Comment