TANGAZO


Monday, August 19, 2013

Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal afungua kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani kuhusiana na suala la Makazi , jijini Arusha leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. (Picha zote na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Ukumbi wa Bunge la Afrika Mashariki, baada ya kufungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, lililofunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. 
Baadhi ya wabunge na wageni waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano hilo leo, jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Maonyesho ya Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. Kulia ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makzi, Prof. Anna Tibaijuka.
 Baadhi ya wabunge na wageni waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano hilo leo, jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Maonyesho ya Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. Kulia ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.
 Baadhi ya wabunge na wageni waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano hilo leo, jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Tree Ltd ya Arusha, Magdalena Ayo, kuhusu utengenezaji wa Majiko Bomba, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, lililofunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. 


Na Richard Mwangulube/ Arusha
Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal leo, amefungua mkutano wa kwanza wa Makazi ulioandaliwa na Jumuiya  ya afrika ya Mashariki (EALA) Mjini Arusha huku akisema suala la makazi mijini ni changamoto kubwa linalozikabili nchi za bara la Afika. 
 
Makamu wa Rais amewambia wabunge zaidi ya 150  wanaoshiriki mkutano huo kwamba  ili kukabiliana na changamoto hizo Serikali katika nchi za Bara la Afrika ni lazima ziwekeze  raslimali nyingi katika suala la makazi mijini ili kukabiliana na chgangamoto ya kuwepo na makazi holela pamoja na mazingira duni.
 
Dakta Bilal amesisitiza umuhimu kwa  nchi za bara la Afrika kuwa na mipango mizuri ya  makazi ili kuwepo na mipangilio mizuri ya ujenzi, miundo mbinu na amewataka wabunge   wanaoshiriki mkutano huo kuangalia  mambo yaliyofanyika katika miaka  25 ya utekelezaji wa malengo ya Melenia (MDGs), kasoro zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wake na miakakti ya kukabiliana nazo.
 
Aidha, Dakta Bilal amewataka wabunge hao kuacha  kuwa  wakosoaji katika Serikali zao tu bali ni lazima  wasaidie kuwa wabunifu katika kuandaa mipango mizuri ya mipango miji.
 
Amesema suala la makazi mijini ni moja ya mahitaji muhimnu ya  binadamu  ambalo linahitaji mtazamo mzuri, uratibu wa karibu .Hata hivyo amesema  hadi sasa katika karne ya 21   bado makazi mengi yamejengwa kwa nyumba za miti, udongo na kuezekwa kwa majani.
 
Dakta Bilal amesisitiza kuwa Serikali ya Tanzania  imechukua hatua  mbalimbali za  kukabiliana na changamoto za  mipango holela na  ujenzi holela,  ambapo pia kumekuwepo na kukosekana kwa huduma zote muhimu za upatikanaji wa majisafi  na salama, hudua za afya na uduni wa  mazingira.
 
Akizungumza katika mkutano huo Rais wa UN-Habitat Barani Afrika   ambaye pia ni Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki  Margaret  Nantongo Zziwa amesema mipango duni,kukosekana kwa maji safi na salama, kukosekana kwa uwekezaji wa kutosha na msongamano  wa makazi ni changamoto kubwa inazikabili nchi za bara la afrika pamoja na mazingira duni.
 
Spika Zziwa amesisitiza kwama  bara la Afrika kamwe haliwezi kuw ana  ushindani katika dunia  kama  watu  wake  wanaishi kwenye mazingira machafu  na makazi duni
Amesema  kama Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ( EAC) ni  yetu ni kuhakikisha    inaboresha  huduma mbalimbali zinazotolewa kwa  watu  wetu kwa kuwepo  na makazi bora,na  huduma  nzuri   za afya pamoja na upatikanaji wa maji  safi na salama
Waziri wa  Ardhi  Nyumba na Makazi wa Tanzania Prof Anna Tibaijuka amesema suala  la mazi mijini linahitaji utashi mkubwa wa kisiasa ili kukabiliana  na chanagamoto mbalimbali.
 
Amesema asilimia 50 ya makazi barani Afrika  haiku katika mpangilio mzuri  hali ambayo inatokana na kukosekana kwa  mipango mizuri  ya mipango miji.
 
Amesema katika nchi za  afrika  hakuna  mipango miji mizuri na kuwataka wananchi kuheshimu  sheria hata hivyo nchi nyingi za  afrika  hazijawa na mipango miji mizuri  ambapo  watu wanadhani  ujenzi   wa miji ni sawa na ujenzi wa vijijini.
 
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira James Daud Lembeli amesisitiza kuwa  masuala ya ardhi hapa Tanzania ni mali ya Tanzania na sio Jumuiya ya Afria ya Mashariki.
 
Mbunge Lembeli amesisitiza kuwa    suala la siasa  lisichukue  nafasi katika upangaji wa mipango miji katika nchi za  Afrika.Hata hivyo amesema  lipo tatizo  la baadhi kutoheshimu sheria za mipango miji, kuvamia  maeneo ya wazi na ambayo  yanalindwa na Sheria.
 
Amesitaka Serikali kuhakikisha  sheria za  ardhi zinasimamiwa kwa nguvu zote na mamlaka husika bila kuingiliw ana wanasiasa.

No comments:

Post a Comment