Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akipewa shada la maua na Afisa Habari Mkuu Idara ya Habari, Bi. Mwanakombo Jumaa kama pongezi kwa kupewa cheo cha Katibu Mkuu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akipongezwa na Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari, Raphel Hokororo alipokuwa akikaribishwa rasmi katika ofisi za Wizara leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga kulia akiwa ameshikana mkono na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Seth Kamuhanda.Tukio hili limefanyika leo jijini Dar es Salaam baada ya makabidhiano rasmi ya ofisi.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Seth Kamuhanda (kushoto), akikabidhiwa zawadi ya picha kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara hiyo Profesa Hermas Mwansoko (kulia), leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kupokea viongozi wapya na kukabidhi ofisi. Kulia ni Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo wakifurahi wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo ambao wameteuliwa hivi karibuni.
Aliyekuwa Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Seth Kamuhanda akitoa hotuba
fupi ya kukabidhi cheo kwa Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (hayupo pichani). (Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo)
Na Magreth Kinabo – Maelezo
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Seith Kamuhanda amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuwateua viongozi ambao ni majembe (wachapakazi) kuiongoza wizara hiyo huku akisema ni watendaji wenye uwezo wa hali ya juu.
Viongozi walioteuliwa kuongoza wizara hiyo ni Sihaba Nkinga ambaye ni Katibu Mkuu wa sasa na Naibu Katibu Mkuu wake ni Profesa Elisante ole Gabriel Laizer.
Kauli hiyo imetolewa leo na Kamuhanda wakati akiwaga viongozi wa wizara hiyo ambapo pia aliwasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha huduma wanazozitoa kupitia sekta za habari, vijana, utamaduni na michezo zinawafikia wananchi.
“Leo ni siku ya furaha kwangu kwa sababu ninaacha majembe mawili ya uhakika. Ninawaomba mwuwape ushirikiano ili walime vizuri. Ni wizara ngumu kwa sababu inagusa Watanzania wote ,”alisema.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa sasa Sihaba alisema anamshukuru Kamuhanda kwa kumfundisha kazi katika maeneo mbalimbali ya sekta za wizara hiyo.
“Nimekaa katika kiti hiki bila ya yeye nisingeweza kukaa katika kiti hiki bado ataendelea kuwa msaada kwangu kwa kuwa wizara inagusa jamii ,” alisema Katibu Mkuu Sihaba huku akimwomba aendelee kutoa msaada katika wizara hiyo.
Aidha Katibu Mkuu huyo alisema atajitahidi kuongoza wizara ili iendelee kuwa watoto wa familia moja kama ilivyoachwa na Kamuhanda.
Naye Naibu Katibu Mkuu Profesa Laizer alisema anamshukuru Kamuhanda kwa ushirikiano aliowapo ,pia aliongeza kuwa kufanya kazi kwake vizuri kutokana na ushirikiano huo ukiwemo wa wakurugenzi ,viongozi wa taasisi na watumishi wa wizara hiyo.
“Kazi kubwa niliyonayo ni kumsaidia Katibu Mkuu. Nitawasaidia ili tupate Matokeo Makubwa Sasa. Tutajitahidi tusikuangushe,” alisisitiza Profesa Laizer huku akisema wao ni majembe lakini yeye ni shoka na ametoka katika wizara hiyo kwa heshima.
Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya menejimenti ya wizara hiyo Profesa, Hermans Mwansoko alimpongeza Kamuhanda kutokana na utendaji kazi wake wakati akiiongoza,ambapo alisema ameiacha katika hali ya umoja na mshikamano huku akiwajali watumishi hususan wa ngazi za chini.
No comments:
Post a Comment