TANGAZO


Monday, July 8, 2013

Waziri Membe: Tunawaunga mkono India na Japan Baraza la Usalama la UN



Kaimu Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia, Omar Mjenga, akizunguza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India, Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Preneet Kaur na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akizungumza wakati alipokuwa akiuufungua mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India, Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Preneet Kaur. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Preneet Kaur  akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India, Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, mara baada ya kuufungua mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India. Kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Preneet Kaur. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Preneet Kaur  akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, mara baada ya kufunguliwa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akifurahi jambo na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Preneet Kaur, Dar es Salaam leo, mara baada ya kuufunguliwa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Preneet Kaur (waliokaa), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India, mara baada ya kuufingua Dar es Salaam leo.



Na Frank Shija – MAELEZO

TANZANIA inaziunga mkono nchi za India na Japan katika 

uwakilishi wa Balaza la Usalama la Umoja wa Taifa.

Hayo yamebaunishwa na Waziri wa Mambop ya Nje na 

Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe alipokuwa akifungua mkutano wa nane wa Kamisheni ya Uhusiano baina ya India na Tanzania  leo, jijini Dar es Salaam.

Waziri Membe amesema kuwa Tanzania inaunga mkono 

nchi za India na Japan ambazo zinawania nafasi ya ujumbe 

wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.


Membe ameongeza kuwa pamoja na kuwa Tanzania 

inaunga mkoni India na Japan katika kupata nafasi ya 

ujumbe katika Balaza hilo na kuwata pia na wao kusaidia 

Bara la Afrika ili liweze kupata nafasi mbili za ujumbe wa 

kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.


“Tunaunga mkono India na Japan kuwa wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lakini niwaombe tu na nyie mtusaidi Afrika ili tupate nafasi mbili za ujmbe wa kudumu katika Baraza la Usalama”. Alisema Waziri Membe.

Aidha Waziri Membe alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali ya 

India kurejesha usafiri wa ndege ya Air India ambao 

ulisitishwa mwaka 2008 na kusema kuwa kwa kufanya hivyo i
tasaidia kufungua fursa za kibiashara na kurahisha usafiri 

kwa wagonjwa wanaopelekwa India kwa matibabu.


Kwa upande wake Waziri wa nchi anayesimamia Mambo ya 

Nje wa Jamhuri ya India Bibi Preneet Kaur amesema kuwa 

Tanzania imekuwa na mahusiano mazuri na nchi ya India 

hivyo mkutano huu ni muendelezo wa mahusiano mazuri 

yaliyoasisiwa na viongozi waliotangulia.

Waziri huyo aliongeza kuwa nchi yake itaendelea 

kushirikiana na Tanzania na kupitia sekta mbalimbali 

ikiwemo Afya,Technolojia na Utamaduni.

Mkutano huu nane wa Kamisheni ya Mahusiano baina ya 

India na Tanzania unajadili mahusiano katika Nyanja za 

Uwekezaji, Elimu, Afya, Utamaduni na Sayansi ya Teknolojia 

na Habari.

No comments:

Post a Comment