TANGAZO


Wednesday, July 17, 2013

Wananchi Rorya, Sumbawanga, Muheza na Njombe watoa maoni Rasimu ya Katiba

MABARAZA ya Katiba ya Wilaya yanayoendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba yanaendelea na kazi ya kujadili na kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume. Mikutano hii ilianza tarehe 12 Julai mwaka huu na inatarajia kumalizika tarehe 12 Septemba, 2012. Pichani, wakazi wa baadhi ya maeneo wakiendelea na mikutano hiyo...


Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Muheza wakijadili na kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wilayani hapo jana (Julai 16, 2013).
Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Mji wa Njombe wakijadili na kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wilayani hapo jana (Julai 16, 2013).
Wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Rorya katika ukumbi wa mkutano wilayani humo muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa kujadili na kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo uliitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Julai 14, 2013.

Mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Rorya Bi. Pendo Bernard, akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Wilayani hapo Julai 14, 2013.
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Bi. Faustina Vallery akitoa kuhusu maadili katika Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wilayani hapo juzi, Julai 14, 2013.

No comments:

Post a Comment