TANGAZO


Monday, July 8, 2013

Papa Francis awakumbuka wahamiaji Italia


Papa Francis amewakumbuka mamia ya wahamiaji wanaokufa maji wakitaufa maisha mazuri Italia
Papa Francis amesherekea maisha ya mamia ya wahamiaji wa kiafrika waliokufa maji wakijaribu kufika baya Ulaya. Akiwa ziarani katika kisiwa cha Lampedusa Papa aliabiri mtumbwi mdogo na kuweka shada la maua ndani ya bahari ya shamu. Kisha alifanya dua ya pakee. Baadaye amekutana na baadhi ya wahamiaji.
Ziara hii ya papa nje ya mji wa Vatican haina mbwembwe, aliwasili kisiwa kidogo ambacho kimekua makao ya maelfu ya wahamiaji haramu wa Kiafrika na kisha baadaye kutumia mtumbwi kuelekea baharini.
Akiwa kwenye bahari ya shamu Papa ameweka shada la maua ya njano kama ishara ya kuwakumbua maelfu ya wahamiaji haramu ambao wamekufa maji wakijaribu kufika kisiwa hicho, kinachotumiwa kama kivukio kwenda barani Ulaya.
Katika bandari ya kisiwa hicho papa amesherekea ibada maalum na baadhi ya wahamiaji na kisha baadaye kurejea makao makuu ya Vatican.
Papa Francis ni mwanawe mhamiaji kutoka Italia ambao waliishi nchini Argentina. Akiwa Askofu mkuu wa Buenes Aires alilaani unyanyasaji wa wahamiaji na kufananisha dhuluma hizo kama utumwa.

No comments:

Post a Comment