TANGAZO


Saturday, July 20, 2013

Mpambano wa Timu za Simba ya Tanzania na URA ya Uganda, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo, Simba yalala 2-1.


Wachezaji wa Simba ya Tanzania na URA ya Uganda wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati yao, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya wachezaji wa akiba wa Simba waliokuwepo benchi wakiangalia kinachoendelea uwanjani hapo.

Kikosi cha timu ya Simba kilichopambana na URA ya Uganda leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Kikosi cha timu ya URA ya Uganda, kilichojitupa Uwanja wa Taifa kupambana na Simba leo jioni.

Waamuzi wa mchezo huo, wakiwa na makapteni wa timu hizo kabla ya kuanza kwa mchezo leo.
Zahoro Pazi wa Simba, akikimbia na mpira huku akifuatwa na Dereck Waluliya wa timu ya URA ya Uganda wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya timu hizo, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. URA ilishinda mabao 2-1. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

 Marcel Boneventura wa Simba akijaribu kumtoka Dereck Waluliya wa URA katika mchezo huo.
 Marcel Boneventura wa Simba akijaribu kumtoka Dereck Waluliya wa URA katika mchezo huo.



 Betram Mombeki wa Simba akishangilia goli aliloifungia timu yake hiyo.
Betram Mombek wa Simba akishangilia goli aliloifungia timu yake hiyo.
Wachezaji wa Simba wakishangilia goli lao la pekee katika mchezo huo, lililofungwa na Betram Mombek (kushoto), wa timu hiyo.
Wachezaji wa Simba wakimpongeza Betram Mombeki wakati wakishangilia goli lao la pekee katika mchezo huo, lililofungwa na mchezaji huyo.





Wachezaji wa URA, wakishangilia goli lao la kusawazisha kabla ya kuongeza la pili na la ushindi kwa timu hiyo dhidi ya wapinzani wao, Simba ya Tanzania leo. 



Kapteni wa timu ya Simba, Nassoro Masoud 'Cholo', akijaribu kumfuata Kasibanti James wa URA ya Uganda kwa ajili ya kumnyang'anya mpira aliokuwa akikimbia nao.
Kapteni wa timu ya Simba, Nassoro Masoud 'Cholo', akijaribu kuzuiya mpira uliopigwa na Kasibanti James wa URA ya Uganda.
Kapteni wa timu ya Simba, Nassoro Masoud 'Cholo', akijaribu kuzuiya mpira uliopigwa na Kasibanti James wa URA ya Uganda.
Hadi mwisho wa mchezo huo, ubao wa matangazo uliokuwa ukionesha Simba 1 na URA 2.

No comments:

Post a Comment