TANGAZO


Tuesday, July 16, 2013

Mkataba wa kuunda mfumo wa kutoa huduma za kitabibu kwa njia ya Eletroniki wasainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Swiss Tropical Public Health Institute

Meneja Mradi waSwiss Tropical Public Health Institute (TPHI), Reinhold Werlein (katikati) akitoa ufafanuzi wa jukumu la taasisi yake  katika mkutano wa kusaini Mkataba wa kuunda Mfumo wa Kutoa Huduma za Kitabibu kwa Njia ya Electroniki kati ya Serikali na taasisi yake uliofanyika ukumbi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mapema leo. Kulia kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi na kushoto kwake ni Mtaalamu wa TEHAMA wa TPHI, Marc Bruner.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi  (kushoto) na Meneja Mradi wa Kampuni itakayotoa Ushauri Elekezi (Consultancy) ya Tropical Public Health Institute, Reinhold Werlein wakisaini mkataba wa Kuunda Mfumo wa Kutoa Huduma za Kitabibu kwa njia ya Elektroniki katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mapema leo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt.Marina Njelekela (kulia) na Meneja Mradi wa kampuni ya Swiss Tropical Public Health Institute (Consultancy Company), wakisaini mkataba wa Kuunda Mfumo wa Kutoa Huduma za Kitabibu kwa Njia ya Elektroniki  katika ukumbi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mapema leo. Waliosimama ni wataalamu wa masuala ya Ugavi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi (kushoto), akikabidhi mkataba wa kuunda Mfumo  wa Kutoa Huduma za Kitabibu kwa njia ya Elektroniki kwa Meneja Mradi wa Swiss Tropical Public Health Institute, Reinhold Werlein katika ukumbi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mapema leo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi akikabidhiwa mkataba wa Kuunda Mfumo wa Kutoa Huduma za Kitabibu kwa njia ya Elektroniki na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Marina Njelekela (wa kwanza kushoto) na Meneja Mradi wa Swiss Tropical Public Health Institute, Reinhold Werlein (katikati) katika ukumbi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma. (Picha na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma)

No comments:

Post a Comment